Shirikisho
la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kesho Jumamosi (Septemba 13 mwaka huu)
saa 4 asubuhi litaendesha mafunzo ya matumizi ya tiketi za
elektroniki kwa wadau wa mpira wa miguu Dar es Salaam.
Mafunzo
hayo Uwanja wa Taifa, na
kushirikisha wasimamizi wa mechi, viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa
Dar es Salaam (DRFA) na makatibu na maofisa habari wa klabu za Azam na
Yanga.
Washiriki wengine
wa mafunzo hayo ni Meneja wa Uwanja wa Taifa na msaidizi wake,
wasimamizi wa milangoni (stewards), waandishi wa habari wa Dar es Salaam maofisa usalama wa TFF.
Mafunzo
hayo yatahitimishwa Jumapili (Septemba 14 mwaka huu) kwa mechi ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga kuanzia saa 10 kamili
jioni.
Tiketi zimeanza kuuzwa jana (Alhamisi)
kupitia M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka ya Fahari Huduma.
BONIFACE WAMBURA
MKURUGENZI WA MASHINDANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
EmoticonEmoticon