Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa nne kushoto)
akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WENTWORTH
inayochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara , Robert MacBean
(wa tatu kushoto) mara baada ya kusaini Makubaliano ya Mkataba wa
Kuuziana Gesi kati yake na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania
(TPDC). Wengine katika picha ni baadhi wa Watendaji Wakuu wa Wizara ya
Nishati na Madini, Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC na
wawakilishi wa kampuni za WENTWORTH na MAUREL & PROM.
Wajumbe
waliohudhuria kikao cha Kusaini Mkataba wa Kuuziana Gesi kati ya
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kampuni zinazochimba
gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara za WENTWORTH Resources
Limited na MAUREL & PROM wakisaini MKataba huo. Anayeshuhudia mbele
ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na
wawakilishi wengine kutoka kampuni hizo, TPDC, Wizara ya Nishati na
Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC) na Kampuni zinazochimba gesi katika eneo la Mnazi Bay
Mkoani Mtwara za WENTWORTH Resources Limited na MAUREL & PROM
zimesaini Mkataba wa Makubaliano wa kuuziana Gesi, ambapo kampuni hizo
zitaingiza gesi hiyo katika visima vilivyopo Mnazi Bay Mtwara kwa ajili
ya Mradi wa Bomba la Gesi.
Kikao hicho cha Makubaliano
kimeongozwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Wizarani ambapo Waziri Muhongo amesisitiza kuwa, Mkataba huo ni fursa
nyingine ya Kiuchumi kwa Tanzania na kuongeza kuwa, Serikali imeazimia
kuingia katika biashara ya gesi na hivyo imedhamiria kufanya biashara
yenye maslahi kwa taifa na iko makini katika usimamizi na utekelezaji wa
biashara hiyo.
EmoticonEmoticon