KUSHOTO NI RAIS JAKAYA KIKWETE AKISALIMIA NA MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO MKOANI TANGA,ALHAJ MAJID MWANGA WAKATI ALIPOFANYA ZIARA WILAYANI HUMO. |
NA MWANDISHI WETU,LUSHOTO.
KIKUNDI cha Ufugaji wa Nyuki na Hifadhi ya Mazingira cha Mwamboa kilichopo Kata ya Mwangoi wilayani Lushoto mkoani Tanga kimepanga kutoa mafunzo kwa vijana wa kike na wa kiume kwenye fani za ufundi seremala kwa ajili ya kutengeneza mizinga ya kisasa,uchakataji wa asali na Nta ifikapo Juni 2015.
Wakiwa na madhumuni ya kutoa ajira kwa vijana wasiopungua 20 lengo likiwa kuwakomboa na limbi la umaskini pamoja na kuwaepusha kukaa vijiweni ambapo hutumia muda mwingi kufanya vitendo viovu kwenye jamii zao ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.
Hayo yalielezwa na Ofisa Ugani wa Kata hiyo, Julius Mshauri wakati akizungumza na blog hii ambapo alisema kuwa licha ya hivyo wamepanga kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kutoka kilo 1,000 iliyopo sasa hadi kufikia 2,500 ifikapo Juni 2015.
Mashauri alisema kuwa katika kuhakikisha jambo hilo linapata mafanikio tayari wamekwisha kustawisha miche ya miti ya aina tofauti tofauti ipatayo 15,000 na kuiuza kwa wananchi kulingana na mahitaji yao ikiwemo kuigawa kwa wanavikundi kwa lengo la kuhifadhi mazingira wakati msimu wa mvua unapoanza mwaka huu.
Akizungumzia chimbuko la kikundi hicho alisema kuwa ni mradi wa
utafiti wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo kupitia program yao
ijulikanavyo ASARECA(Associationfor Strehgttening Agricultural
Research in Eastern and Central Africa).
Alisema kuwa ndani ya program hiyo kikundi hicho kimeweza kushiriki kwenye mafunzo ya aina mbalimbali hasa ya ufugaji bora wa nyuki na utafutaji wa masoko kwa kushiriki kwenye maenyesho hususani ya kibiashara ya kimataifa na pia yale ya nanenane.
Ofisa ugani huyo alisema kikundi hicho kilipata ufadhili kutoka
serikali ya Poland kwa kupitia shirika la Poland East Africa Economic Foundation ambapo waliweza kufanya nao kazi kwa kipidi cha mwaka mmoja.
Hata hivyo alisema kuwa ndani ya kipindi hicho walifanya mambo
mbalimbali ikiwemo ujenzi wa kituo cha kikundi hicho ambapo ujenzi huo uligharimu kiasi cha sh.milioni 45 zilitumika mbali na nguvu za wananchi zilizotumika kwa wanakikundi zilikuwa ni tsh milioni 9.

EmoticonEmoticon