NA MWANDISHI WETU,TANGA.
TIMU YA African Sports “Wanakimanumanu “jana ilianza
vema maandalizi ya kuelekea michuano ya Ligi daraja la kwanza baada ya
kuibamiza timu ya Maafande wa Jeshi la Magereza mkoani hapa Small Prison mabao
2-0.
Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa kwenye uwanja wa
CCM Mkwakwani na kushuhudiwa na mashabiki mbalimbali wa soka mkoani hapa.
African Sports iliyopanda daraja msimu huu na
kufanikiwa kucheza ligi daraja la kwanza ikwisha kucheza michezo mbalimbali ya
majaribio ili kuweza kukipa makali kikosi hicho ambacho kitashiriki ligi hiyo
kwa mara ya kwanza tokea iliposhuka daraja miaka.
Katika mchezo huo bao la kwanza la African Sports
lilifungwa dakika ya 42 kupitia Mohamed Farid ambaye aliweza kutumia uzembe wa
mabeki wa wapinzani wao kupachika wavuini bao hilo kabla ya timu hizo
haijakwenda mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo timu zote
ziliingia uwanjani zikiwa na nguvu mpya baada ya kufanya mabadiliko kwa baadhi
ya wachezaji wao.
Wakionekana kujipanga kwwenye mchezo huo, African
Sports waliweza kuongeza wimbi la mashambulizi langoni mwa timu pinzani hali
iliyopelekea kuongeza bao la pili ambalo lilifuingwa na Evalisti Joseph ambaye
alimaliza kazi nzuri iliyofanywa na Mohamed Farid.
Akizungumza baada ya kumalizika mchezo huo,Ofisa
Habari wa timu ya African Sports ,Saidi Karsandas alisema kuwa mipango ya timu
hiyo ni kucheza mechi nyingi za majaribio ili kuweza kukiweka kikosi hicho
imara kwa ajili ya michuano ya ligi daraja la kwanza.
EmoticonEmoticon