Angel di Maria akiwa kwenye picha ya pamoja na Bosi wake Mpya wa Manchester United Louis van Gaal
Di Maria amesaini Mkataba wa miaka 5.
MANCHESTER UNITED imetangaza rasmi kuwa Angel Di Maria amekamilisha Uhamisho wake kwa Dau la Rekodi huko Uingereza la Pauni Milioni 59.7 akitokea Real Madrid ya Spain.
Mara baada ya kukamilisha taratibu za Uhamisho, Di Maria alisema: “Nina furaha kupita kifani kujiunga na Manchester United. Nilikuwa na raha kule Spain na Klabu nyingi zilinitaka lakini Man United ndio Klabu pekee ningeweza kuiacha Real Madrid ili kujiunga nayo.
Louis van Gaal ni Kocha bora sana mwenye
rekodi nzuri na nimevutiwa mno na dira na nia ya kila Mtu Klabuni hapa
ili kuirudisha tena juu ambako ndiko inastahili kuwepo. Nani hamu kubwa
kuanza kazi!”
Nae Meneja Louis van Gaal, akimkaribisha Di Maria, amesema: “Angel ni Kiungo wa kiwango cha Dunia lakini muhimu zaidi ni Mchezaji Kitimu. Hamna shaka kuhusu kipaji chake kisicho mfano. Ni mwepesi sana na hatari kwa Guu la Kushoto ambae anatisha Difensi yoyote ile. Uwezo wake kukokota Mpira na kuwakabili Mabeki na kuwadaa ni kitu cha furaha kukiangalia. Ni nyongeza safi sana kwa Timu!”

Di Maria akimwaga wino kusaini Mkataba na Klabu ya Man United na hapa alikuwa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Ed Woodward.
EmoticonEmoticon