KLABU ya Barcelona imekubali kumsajili beki wa kulia Douglas Pereira kutoka Sao Paulo kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 3.19, vigogo hao wa Katalumya wamethibitisha jana.
Uhamisho
unaweza kupanda kwa Pauni Milioni 1.2 zaidi kwa ajili ya beki huyo
mwenye umri wa miaka 24 kulingana idadi ya mechi atakazocheza katika
klabu yake mpya.
Pereira atajiunga na klabu hiyo ya La Liga kwa mkataba wa miaka mitano iwapo atafaulu vipimo vya afya wiki hii nchini Hispania.
EmoticonEmoticon