Mwenyekiti wa Bunge Maalum Samuel Sita akiongoza kikao cha
Kamati ya Uongozi cha Bunge hilo kilichokaa leo
Jumatatu Agosti 4, 2014, kupanga ratiba ya Bunge hilo
linaloanza Jumanne, Agosti 5, 2014 mjini Dodoma. Bunge hilo linaanza baada ya kuahirishwa Aprili 25,
mwaka huu, ambapo wajumbe wanaotoka vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi
wengi wao wakiwa ni wafuasi wa vyama vya upinzani, waligomea mchakato huo ambao
ulikuwa umefikia hatua ya kupiga kura ya
kupitisha vipengele vilivyojadiliwa tayari kikubwa kikiwa ni muundo wa
serikali. UKAWA inasisitiza kuwepo kwa muundo wa serikali tatu, wakati wajumbe
wengine wengi wao wakiwa ni wale wa chama tawala CCM, wakiweka msimamo wa
kuendelea na mfumo wa sasa wa serikali mbili.
|
EmoticonEmoticon