Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred
akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoa elimu kwa wajasiliamali kwa
albino 50, kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa Jumuiya wa watu wenye ulemavu wa
ngozi (albino), Mohamed Chanzi.
Kaimu katibu Mkuu wa Jumuiya wa watu wenye
ulemavu wa ngozi (albino), Mohamed Chanzi (Kushoto) akisisitiza jambo katika
uzinduzi wa mpango huo. Wengine katika picha ni Brigitte Alfred (katikati) na
Maria Ngowi ambaye ni mkurugenzi wa JAT
Viongozi wa Taasisi ya Brigitte Alfred
Foundation, TAS na JAT katika picha ya pamoja mara baada ya kuzinduzi mpango wa
kusomesha albino 50 masomo ya Ujasiriamali.
***********
Na Mwandishi wetu
Taasisi ya ya Miss Tanzania 2012, Brigitte
Alfred ijulikanayo kwa jina na Brigitte Alfred Foundation (BAF) ikishirikiana
na taasisi ya Junior Achievement Tanzania (JAT) inazindua rasmi mafunzo ya
ujasiriamali kwa jamii ya Albino.
Akizungumza katika uzinduzi huo jana,
Brigitte alisema kuwa taasisi yake kwa kushirikiana na JAT itaanza na mafunzo
kwa albino 50.
Brigitte alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga
sehemu kuu mbalimbali ambazo ni kujitambua (Life skills), kutathmini aina
mbalimbali za biashara (Business Analysis), namna ya kutunza pesa ( How to
save), kuandika mchanganuo wa biashara (Business Plan), kutembelea sehemu
mbalimbali zinazoendana na biashara atakayoifanya na jinsi ya kuanza biashara.
Alisema kuwa BAF ikishirikiana na wadau
mbalimbali na pia itagharimia gharama za mafunzo na mahitaji mbalimbali ya
kuboresha hali yao.
“Mafunzo haya yatachukua muda wa mwaka mmoja
yaani watashiriki na yataanza rasmi Agosti 18, kila mshiriki wa mafunzo haya
atapatiwa kitabu chenye masomo yote ili aweze kuendelea kujisomea,” alisema
Brigitte.
Mkurugenzi wa JAT, Maria Ngowi alisema kuwa
wamejipanga kufanikisha mpango huo na wanaamini albino watakaopata mafunzo hayo
watafanikiwa katika maisha yao ya kila siku.
Ngowi alisema kuwa JAT imejikita katika
Nyanja tatu ambazo ni ujasiria mali, elimu ya kuzalisha, kuiwekeza na kutunza
fedha na elimu ya kazi.
Alisema kuwa taasisi yao ni sehemu ya taasisi
kubwa ulimwenguni inayoitwa Junior Achievement International ambayo iko katika
nchi 120 duniani huku afrika ikiwa katika nchi 17.
Kaimu Katibu Mkuu wa Tanzania Albino Society
(TAS), Mohamed Chanzi alimshukuru Brigitte na JAT kwa kuwajali na kuomba wadau
mbali mbali kuwaunga mkono.
“Wamelenga kutusaidia kimaisha, kwani msaada
wa elimu ni mkubwa kulinganisha misaada mingine, naomba wadau wawaunge mkono,”
alisema Chanzi.
EmoticonEmoticon