YULE POLISI FEKI USALAMA BARABARANI ALIYEKAMATWA CHAMAZI, MBAGALA AANIKWA WAZI NA KOVA!!

August 04, 2014

Kamishna Kova (katikati) akionesha kidole kwa polisi feki aliyekamatwa.

Sura ya ‘karibu’ ya askari huyo feki aliyekamatwa.

Kova akionyesha baadhi ya sare za jeshi la polisi alizokamatwa nazo polisi huyo feki.
Waandishi wa habari waliokuwa katika tukio hilo.

JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam linamshikilia na kumhoji mtu mmoja anayeitwa Robson Seif Mwakyusa (30) mkazi wa Kijitonyama Jijini Dar, kwa tuhuma za kujifanya ofisa wa polisi kikosi cha usalama barabarani  hukuakifanya ukaguzi wa makosa ya usalama barabarani
Mtuhumiwa huyu alikamatwa jumamosi  iliyopita huko Kata ya Chamazi, Mbagala-Majimatitu Mkoa wa Kipolisi Temeke akiwa amevalia sare za polisi na cheo cha stesheni sajenti na akiwa na leseni mbalinbali za magari, ‘radio-call’, stakabadhi, na vitu vingine.
Na Gabriel Ng’osha/GPL

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »