Scott
Eisner (kulia)vice President of African Affairs, US Chambers of
Commerce akifungua sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza Afrika 2014
iliyofanyika US Chambers of Commerce Washington, DC siku ya Jumatatu May
19, 2014 wengine katika meza ni Balozi wa kudumu wa African Union Mhe.
Amina Salum Ali na Paul Duffen ambaye ni News Desk Media.
Sherehe
ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza afrika 2014 ".invest in africa 2014"
kitabu kinachotolewa na ubalozi wa umoja wa afrika ilifanyika Jumatatu
May 19, 2014 kama kuanzia wiki ya kusherehekea siku ya afrika tarehe 27
mwezi mei .
Katika
sherehe hizi zilizoandaliwa kwa pamoja baina ya ubalozi wa afrika
washington na jumuia ya wafanya biashara wa marekani US chamber of
commerce
Kulikuwa
na majadiliano yaliyofanywa na viongozi wanao wakilisha Mabalozi wa
kanda 5 za afrika zikiwemo East.West .South Central na North.viongozi
hao walizungumzia rasilmali zilizopo Afrika na kuwaalika wawekezaji
wawekeze afrika kwani kuna faida kubwa zinapatikana. Kwa upande wa
serikali ya marekani ilihudhuriwa na mwakilishi wa msaidizi katibu wa
ofisi ya mambo ya nje ya marekani na mgeni mwengine wa heshima ni
muwakilishi wa umoja wa matIfa united nation global compact.kitabu
kilichotoka mwaka huu pia kimeelezea mafanikio yaliyopatikana afrika na
muelekeo katika miaka ijayo.
Sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza Afrika 2014 ikiendelea.
Meza upande wa wawekezaji
Meza waliokaa wawakilishi wa serikali ya Marekani
Mwakilishi wakiendelea na sherehe ya uzinduzi wa kitabu cha wekeza Afrika 2014.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula(kushoto) katika
picha ya pamoja na Balozi wa kudumu wa African Union Mhe. Amina Salum
Ali na Danille Walker ambaye ni Director of African Affairs, US Chambers
of Commerce
Afisa Ubalozi Suleiman Salehe katika picha ya pamoja na Balozi wa Ivory Cost nchini Marekani Mhe. Daouda Diabate
picha ya pamoja waheshimiwa Mabalozi, Maafisa na wawakilishi wa Mabalozi
EmoticonEmoticon