MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM),Abdi
Makange amewataka wanafunzi katika vyuo mbalimbali hapa nchini kuacha kufikiria
masuala ya migomo na maandamano badala yake waone namna ya watakavyo jiajiri wakati
watakapokuwa wamemaliza kwenye vyuo hivyo.
Makange alitoa wito huo mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali
ya Chuo cha kujiendeleza kielimu
cha Noverty kilichopo mjini Tanga ambapo alisema masuala hayo
hayana faida yoyote kwao zaidi ya kuwaharibia malengo yao
waliyojiwekea kwenye maisha yao
ya baadae.
Alisema ni vema wakamua njia za busara kuiepuka migomo na
maandamano yasiyo na tija kwenye vyuo vyao lengo likiwa kukaa chini na
kuzungumza ili kuweza kupata muafaka badala ya kujichukulia hatua za aina hiyo
kwani sio suluhu ya kile wanachokuwa wakikitaka zaidia ya kuwapa hasara jamii zao wanazotoka.
Alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa chuo hicho kwa
kutoa elimu kwenye jamii ndio maana wamekuwa wakiwaalika kwenye matamasha na
vikao mbalimbali ikiwemo baadhi ya misaada wanayoipeleka.
Aidha alisema chuo hicho kimekuwa mkombozi mkubwa wa vijana
kwa kuwawezesha kupata ajira kwenye sekta mbalimbali mkoani hapa kitendo
ambacho kinachangia kukuza maendeleo yao
na jamii zinazowazunguka.
Akilizungumzia suala la Katiba,Makange alisema nchi imeingia
kwenye mchakato wa katiba mpya ambapo itakayoandikwa leo itaishi miaka 59 ijayo
na walengwa ni vijana hivyo wahakikisha wanakataa mambo ambayo yanaweza
kuwagawa watanzania na mshikamano wao.
Mwenyekiti huyo aliwataka pia wahitimu hao kuhakikisha
wanakuwa mabalozi wazuri kwenye jamii wanazoishi pamoja ikiwemo kuwaasa wanafunzi
wa kike kujiadhari na mafataki ambao wanaweza kuwaharibia maisha yao hali itakayowafanya kushindwa kufikia malengo yao.
“Hakikisheni mnakuwa
mabalozi wazuri kwenye jamii zenu lakini kwa upande wa wasichana napenda
kuwaasa mjihadhari na mafataki wanaoweza kuwaharibia malengo yenu ikiwemo
wanafunz mnaobaki tilieni mkazo elimu kwani ndio njia pekee itayowaletea maisha
bora “Alisema Makange.
EmoticonEmoticon