NA BONIFACE WAMBURA,DAR ES SALAAM.
Mechi
ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika mwakani nchini Morocco
kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe iliyochezwa Jumapili katika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 63,345,000.
Mapato
hayo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Taifa Stars kuibuka na ushindi wa bao
1-0 yametokana na washabiki 11,079 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa
viingilio vya sh. 5,000, sh. 10,000 na sh. 20,000.
Mgawo
wa mapato hayo ni asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni
sh. 9,662,796.61, gharama za kuchapa tiketi sh. 6,000,000, asilimia 15 ya
uwanja ni sh. 7,152,330.51, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 9,536,440.68
na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) kwa pamoja wamepata sh. 30,993,432.20.
Katika hatua nyengine,Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaandaa utaratibu utakaowawezesha washabiki
kwenda jijini Harare, Zimbabwe kushuhudia mechi ya Taifa Stars.
Mechi
hiyo ya marudiano ya Kombe la Afrika kwa ajili ya fainali zitakazochezwa
Morocco mwakani itafanyika Jumapili (Juni 1 mwaka huu) jijini Harare.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilishinda mechi ya kwanza
iliyochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa bao 1-0.
Usafiri
huo utakuwa wa basi ambapo washabiki wanatarajiwa kuondoka siku ya Ijumaa na
kuwasili Jumapili mchana jijini Harare ambapo watashuhudia mechi na kuanza
safari ya kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo.
Washabiki
wanatakiwa kuwa na hati za kusafiria (pasipoti), nauli ya kwenda na kurudi
itakuwa sh. 300,000.
EmoticonEmoticon