SHILOLE ABADILI JINA LA HOTEL YAKE

May 03, 2014
 

Mwanamuziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amebadilisha jina la Hoteli yake mpya anayotarajia kuifungua maeneo ya Mwananyamala, awali jina la Hoteli hiyo aliiita Chuna Buzi Hotel lakini baada ya ushauri sasa anaipa jina la Igunga One Restaurant.

“Nimeamua kubadili jina baada ya kushauriwa na rafiki zangu, maana jina la kwanza lilikuwa na utata, na hata lilikuwa na maswali mengi kwa wapita njia, lakini jina la sasa lipo poa kila mtu kalifurahia,”anasema

Moja ya sababu nyingine iliyopelekea kubadili jina na kuipa jina la Igunga One Restraurant, ni kutokana na huduma itakayopatikana katika Hotel hiyo kutauzwa vinywaji baridi na vileo, alisema Shilole.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »