MRISHO MPOTO AWALIZA WAANDISHI NA WIMBO WAKE MPYA

May 03, 2014

Msanii Mrisho Mpoto akitoa burudani kwa washiriki wa mkutano unaoenda sanjari na siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza kwa makini msanii Mrisho Mpoto aliyekuwa akiimba wimbo mpya unaohusu waandishi wa habari,wimbo ambao umo katika albamu yake mpya aliyozindua leo .
Jaji Mstaafu Mark Bomani akizundua video mpya ya msanii Mrisho Mpoto ya wimbo wake unaohusu waandishi wa habari , katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha kunako fanyika mkutano unaenda sanjari na siku ya uhuru wa habari duniani.
Washiriki wa mkutano huo wakitizama Video mpya ya Msanii Mrisho Mpoto ya wimbo wake mpya unaohusu waandishi wa habari.
Wimbo mpya wa msanii Mrisho Mpoto uliwatia wengi Simanzi baada ya kutizama Video hiyo.
Msanii Mrisho Mpoto akimkabidhi Mh Jaji Mstaafu Mark Bomani VCD ya video ya albamu yake mpya ijulikanao kama "WAITE"kwa ajili ya uzinduzi.
Mh,Jaji Mstaafu akizindua rasmi albamu ya pili ya msanii Mrisho Mpoto ,Ijulikanayo kama "Waite"
Msanii Mrisho Mpoto akizungumza muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa albamu yake mpya ya WAITE.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »