Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni
mpaka kati ya Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe
mkoani Kigoma leo Alhamisi, Aprili 10, 2014. Kinana yupo katika ziara ya siku tano mkoani humo ya
kukagua uhai wa Chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani humo. Moja
ya kero kwenye mpaka huo unaokutanisha vijiji vya Kibande (Tanzania) na
Murambi (Burundi) ni Watanzania kulazimika kukumbana na adha ya
kuvuka mto huo kwenda kufanya biashara na kununua mahitaji kwenye soko
lililopo upande wa Burundi. Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye

Eneo
la soko la Murambi, Burundi ambako Watanzania hulazimika kwenda
kufanyabiashara na kupata mahitaji huko kutokana na upande wa nchi yao
kutokuwa na soko ikiwemo la mifugo lililokuwepo zamani na sasa halipo
kutokana na kufungwa kwa sababu zisizojulikana, ambaopo Kinana alihoji
kwa nini lisiwepo soko upande wa Tanzania ili kuondoa kero ya watu
kuvuka mto kila siku kwenda ng'ambo.

Juu ya maelezo haya ni wananchi wakivuka mto Malagarasi kutoka upande wa Burundi kuingia Tanzania

Wananchi
wa Kijiji cha Buhigwe wakimlaki Kinana alipowasili kwenye Ofisi ya CCM
Kata ya Buhigwe, kuzungumza na Kamati ya Siasa ya CCM wilayani humo, leo

'Obama' akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa michezo Kata ya Buhigwe.
Katibu Mkuu wa CCm Abdulrahman Kinana akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wananchi wa Buhigwe wakati wa mkutano huo

Nape
akiwa amezungukwa na watoto wa Kijiji cha Kibande, wakati akifanya kazi
zake kwenye kompyuta pambeni mwa mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja
vya Kijiji hicho kata ya Buhigwe

Baadhi ya matangazo kwenye mpaka huo


Kinana akisalimiana na wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Munanila wilayani Buhigwe.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa na Kinana, Munanila, Buhigwe


EmoticonEmoticon