MAKALLA AHIMIZA WATANZANA KUWA WAMOJA .

April 11, 2014

Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla ( suti yeusi ), na Mbunge wa Jimbo la Mvomero, akimkabidhi Katekista, Isaka Manyoni , wa Kanisa Katoliki la Mchungaji Mwema katika Kigango Wami Sokoine fedha tasilmu sh milioni mbili ambazo zimetolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, juzi ikiwa ni kutimiza ahadi yake ya mwaka mmoja uliopita kwa Kwaya ya Muungano wa Kanisa hilo lililojengwa kuenzi mchango wa aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Sokoine , eneo la Wami Sokoine.

Na Mtanda Blog, Morogoro.

KANISA Katoliki na madhehebu mengine nchini yameombwa kuombea Bunge la Katiba ili liweze kujadili rasimu ya katiba iliyopo mbele yao kwa amani ,upendo na uvumilivu ili kuwezesha upatikanaji wa Katiba bora itakayowanufaisha watanzania wote.Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla , kwenye hotuba yake wakati wa ibada ya Jumapili Aprili 7, mwaka huu iliyofanyika katika Kanisa la Mchungaji Mwema , Wami Sokoine , wilayani Mvomero. 

Naibu waziri huyo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mvomero pia alimwakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kukabidhi sh: milioni mbili alizokuwa ameahidi mwaka juzi kwa kwaya ya Kanisa hilo, wakati mwenyewe akichangia haramberee sh: 100,000 kwa ajili ya watoto wa kanisal hilo. 
Awai Kabla ya kukabidhi fedha hizo, alitumia fursa hiyo kuliomba kanisa na madhehebu mengine kutochoka katika kuliombea bunge la katiba kufiatua hali inayoendelea kujitokeza Bungeni hapo. 
“ Kama ilivyo Bungeni kujadili Katiba inahitaji maombezi makubwa ...ili kila mmoja wetu awezakuwa na upendo na uvumilivu ili Tanzania ipate Katiba iliyobora “ alisema Naibu Waziri huyo. 
Mbali na hayo aliwaomba Watanzania kuliombea Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete anaye maliza muda wake ili aiache nchi ikiwa na Katiba Bora kwa manufaa ya watanzania wote. 
Pia Naibu Waziri Makalla alihimiza watanzania waendelee kudumu katika umoja , ushirikianao wakidugu na pia wananchi kupinga kila njama itakayowatumbukiza kwenye masuala la ubaguzi wa dini, rangi na jinsia. 
Hivyo alisema , kwa kudumisha misingi hiyo iliyoazisiwa na waasisi wetu wa Taifa hili, ni wajibu wa kila watanzania kuendeleza umoja huo kwa kizazi cha sasa na kijacho. 
Katika hatua nyingine, Makalla aliwa hakikishia waumini wa Kanisa hilo na maeneo mengine ya karibu watapatiwa umeme muda mfupi ujao mara baada ya Tanesco kukamilisha kuweka nguzo na kusambaza nyaya chini ya mradi wa nishati vijijini ili Kanisa liweza kutumia vifaa vya kisasa kwenye ibada .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »