April 07, 2014

WIZARA YA FEDHA YAWEKA WAZI JINSI ITAKAVYOTEKELEZA MATOKEO MAKUBWA SASA 'BRN'

Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa 'Mablogger', iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park, Misugusugu Kibaha, hivi karibuni. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now).
*************************************************

wizara ya fedha imeeleza wazi kuhusu mipango yake ya kutekeleza matokeo makubwa sasa(BRN) ikiwa ni utraatibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo makubwa kwa muda mfupi
Akieleza malengo hayo hayo msemaji mkuu wa wizara ya fedha, INGIAHEDI MDUMA amesema wizara ya fedha imejipanga Kutafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi kufikia mwaka 2015/16
Pamoja na hayo Mduma amesema pia wamedhamiria kupunguza nakisi katika bajeti ya Serikali kwa shilingi trilioni 4 kufikia mwaka 2015/16 na Kutekeleza miradi ya PPP yenye thamani ya shilingi trilioni 6 kufikia mwaka 2015/16
Malengo mengine ni kuhakikisha kwamba shughuli za BRN zinapatiwa fedha za kutekeleza miradi iliyopangwa ili kuweza kusimamia malengo yaliyokusudiwa 
Aidha amesema viashiria vya utafutaji wa mapato vinavyotekelezwa na Wizara ya Fedha vimegawanyika katika sehemu kuu nne ikiwemo ya mapato ya kodi, mapato yasiyo ya kodi, ubia katika sekta ya umma na sekta binafsi na kudhibiti matumizi ya serikali.
katika kuelezea malengo hayo amesema Katika kipindi cha Julai – Disemba, 2013 jumla ya shilingi bilioni 215.0 zimekusanywa kutokana na hatua mpya za kodi zilizoibuliwa kwenye maabara za BRN. 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »