DC MWANGA AWAPA KAZI MGAMBO.

January 28, 2014
Na Oscar Assenga,Lushoto.

MKUU wa wilaya ya Lushoto,Alhaj Majid Mwanga amewataka vijana
walihitimu mafunzo ya mgambo kata ya Lukozi Tarafa ya Mlalo wilayani humo kufuatilia na komesha vitendo vinavyofanywa na vijana vya kuwapa mimba wanafunzi kike  pamoja na kuwakamata wazazi wanaowaozesha watoto wao wakiwa bado mashuleni.

Mwanga alitoa agizo hilo jana wakati akifunga mafunzo ya mgambo ya
  miezi sita kata ya Lukozi Tarafa ya Mlalo kwa wahitimu wapatao 99 ambapo kati yao wa kike watano na wakiune tisini na nne.

Alisema wahitimu hao wana jukumu kubwa la kuhakikisha pia

wanalidhibiti suala la utoro kwa wanafunzi pamoja na kutoa elimu juu ya athari za ukimwi na rushwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.

Mkuu huyo wa wilaya alisema suala lengine ambalo wanapaswa kulitia
mkazo mkubwa ni kuwaeleza vijana wengine mafanikio yaliyoyapata wakati wa mafunzo  hayo ikiwemo kulinda vyanzo vya maji na misitu.

Aidha aliwataka vijana hao kushiriki katika shughuli mbalimbali za

maendeleo kama ujenzi wa maabara pamoja na kuwa mstari wa mbele kuzuia vitendo viovu kwenye jamii zao ikiwemo wizi,uporaji.

Hata hivyo DC Mwanga aliwataka wahitimu hao kuwa mabalozi wazuri
  kwenye familia zao kupitia kauli mbiu ya Jeshi la Polisi Tanzania ya kuwa “Katika familia yangu hakuna uhalifu na  Utii wa sheria bila shuruti n wa kila mwananchi na kila kiongozi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »