Na Oscar
Assenga,Tanga.
TIMU ya
Coastal Union ya Tanga leo imeshindwa kuutimia vema uwanja wake wa nyumbani
baada ya kulazimishwa sare na Oljoro JKT ya Arusha kwenye mechi ya Ligi kuu
Tanzania bara mzunguko wa
pili.
Mchezo huo
uliochezwa kwenye dimba la soka Mkwakwani ulikuwa mkali na wenye upinzani
mkubwa ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko Coastal Union walikuwa
wakiongoza bao 1-0.
Bao ambalo
lilifungwa na Yayo Lutimba aliyeunganisha pasi nzuri iliyopigwa na Hamadi
Hamisi bao ambalo lilidumu mpaka timu zote zinakwenda mapumziko.
Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi ambapo Coastal Union na Oljoro JKT waliingia kwenye ngwe
hiyo kwa kila timu kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake.
Wakicheza
kwa kujituma na umakini mkubwa Coastal Union waliweza kutawala mchezo huo mpaka
dakika ya 75 ya kipindi cha pili ambapo nao wapinzani wao walipocharuka.
Baada ya
kucharuka Oljoro JKT waliweza kucheza pasi fupi fupi na ndefu wakitumia udhaifu
wa wapinzani wao na ndipo walipofanikiwa kuandika bao la kusawadhisha kwenye
dakika ya 87 kupitia Hamis Salehe.
Hata hivyo
mechi ya leo ilikuwa haina mashabiki wengi kwa kile kilichoelezwa kuwa mfumo wa
kielectroniki ulichangia kuwepo kwa hali hiyo.
Kikosi cha Coastal Union leo gk Said Lubawa,Hamadi Hamisi,Othumani Tamimu,Juma Nyoso,Jerry Santo,Mbwana Hamisi,Atupele Green,Razack Khalifani,Yayo Lutimba,Daniel Lyanga na Keneth Masumbuko.
Kwa upande wa JKT Oljoro gk Mohamed Ally,Paul Malipesa,Ally Omari,Nurdin Mohamed,Sabri Makame,Babu Ally,Jacob Massawe,Azizi Shaweji,Amiri Omari,Shija Mkina na Majaliwa Shabani.
Michezo mengine iliyochezwa kwenye ligi hiyo ni Ashanti United walicheza na Yanga ambapo mpaka dakika 90 Yanga 2-1 Ashanti United.
Mabao ya Yanga yakifungwa na Didier Kavumbangu na David Luhende dakika ya 51 na 82 na la Ashanti United limefungwa Bright Obinna dakika ya 61
Kwenye dimba la Chamazi,Azam Fc waliibika na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar bao likifungwa na Kipre Tchetche.
Hali kadhalika Mbeya City nao waliibuka na ushindi wa Bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye dimba la soka Katiba Bukoba bao hilo likifungwa na Swita Julius
EmoticonEmoticon