TFF,UONGOZI WA UWANJA WA MKWAKWANI WAJIPANGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA KIELECTRONIKI LEO.

January 25, 2014
Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga,Gustav Mubba(kushoto)akizungunza na waandishi wa habari jana na kulia ni Meneja wa uwanja huo,Mbwana Msumari.
Oscar Assenga,Tanga.
Shirikisho la Soka nchini TFF kwa kushirikiana na uongozi wa uwanja wa Mkwakwani limejipanga kubaliana na changamoto zitakazojitokeza katika mchezo wa leo kuhusiana na tiketi za Kielektroniki.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana uwanjani
  hapo,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF,Khalid Abdallah  na katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga,Gustav Muba walisema wamejipanga kukabiliana na changamoto hizo.

Khalid ambaye pia ni msimamizi wa ligi kuu Vodacom,kituo cha Tanga
  alisema baada ya kukamilika kwa matengenezo ya uwanja wa Mkwakwani kuna changamoto ambazo zitajitokeza kutokana na ukweli kwamba milango iliyoandaliwa ni miwili tu.

“Tatizo ni kwamba wawekaji wa mashine za kielektroniki wameweka mageti
  mawili tu ambayo kwa uzoefu ukataji wa tiketi hautatosheleza idadi ya mashabiki watakaoingia”alisema Khalid.


Mjumbe huyo hata hivyo aliwataka wapenzi kujitokeza kwa wingi bila
kuhofia tatizo hilo kwa sababu,TFF na uongozi wa uwanja wamejipanga kuhakikisha kila atakayefika anaingia uwanjani kushuhudia mechi baina ya Coastal Union na Oljoro JKT ya Arusha.

Viingilio katika mechi hiyo ya leo jumamosi katika uwanja wa

Mkwakwani vitakuwa sh 10,000/= na 3000/= ambapo vimeandaliwa vituo zaidi ya saba kwa ajili ya kukatia tiketi za elektroniki.

Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga alisema uwanja wa mkwakwani umekamilika
  marekebisho kwa asilimia kubwa na unaweza kuhimili kuchezewa ligi kuu bila matatizo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »