Na Mbaruku
Yusuph,Tanga.
Imewekwa Desemba 26 saa 12:25 Mchana.
CHAMA cha
Mapinduzi CCM,Mkoani Tanga kimempongeza Mh;Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuridhia
maamuzi ya bunge ya kuwataka Mawaziri
wanne kujiuzulu nyadhifa zao.
Akizungumza
na TANGA RAHA ofisini kwake Katibu wa CCM Mkoa Tanga,Gastav Muba kuwa msimamo uliowekwa na Bunge kwa Mawaziri
hao wanne wa kuwajibishwa ni sahihi kwa lengo la kulinda maslahi ya chama na mwananchi kwa ujumla.
Aidha
alisema kuwa wananchi wanapaswa kufahamu
kila maamuzi magumu yanayochukuliuwa na serikali si kwa utashi wa chama
tu ,bali ni kwa ajili maslahi ya wananchi amabao kwa namna moja au nyingine
ndio wanaoumia.
“Nani hatambui kuwa wananchi ndio
wenye nchi?.Wananchi ndio msingi mkuu wa nchi kwa nini serikali isichukue hatua
kali kwa watumishi wasio waadilifu?”Alihoji bwana Muba.
Muba alizidi
kufafanua kuwa hatua hiyo imekuja muda muafaka kwa Chama kwa kuwajengea imani
wanachama wake ambao ni kundi kubwa linalo pata madhila pindi panapotokea
uvunjifu wa haki za binaadamu hapa nchini
.
Alisema
kitendo cha Mh; Rais kuridhia uwajibishwaji kwa Mawaziri hao ni ukomavu kwa
Chama na kulinda maslahi ya mwananchi kitu ambacho kitakiletea tija chama na
wala si udhaifu katika chama kama habari zinavyo zagaa hapa nchini.
“Unajua ikiwa Waziri au
Mawaziri,wameshindwa kusimamia vema utekelezaji wa majukumu yao na kuwasimamia
waliochini ya wizara zao katika sekta yoyote serikalini,Si udhaifu wa chama
bali ni mapungufu ya mtu mwenyewe binafsi na kujisahau kama amebeba dhima kubwa ya
kuwatumikia wananchi na hakuna sababu ya kuleyana”Alisema katibu huyo.
Hata hivyo
aliwapongeza Wabunge wote bila ya kuangalia tofauti ya vyama vyao,Mawaziri na
Mh: Raisi kwa kubeba dhamana kubwa ya kusimamia vema maslahi ya mwananchi ambae
ndio msingi mkubwa katika chi yoyote duniani.
Aliwaomba
wananchi wote Mkoani Tanga kuwa na imani na chama chao na kuacha kusikiliza propaganda zinazoenezwa mitaani
kuwa chama sasa kimepoteza uwelekeo hakuna kitu kama hicho,kuwajibishwa kwa
Mawaziri hakupelekei kupoteza uwelekeo kwa CHAMA.

EmoticonEmoticon