
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki Moon akimkaribisha Rais Jakaya
Mrisho Kikwete kwenye ofisi yake iliyopo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
jijini New York, Marekani juzi (24/12/2013) .Viongozi hao wawili
walijadili masuala mbalimbali ya kimataifa hususan masuala ya amani na
ushiriki wa majeshi ya Tanzania katika kudumisha amani sehemu mbalimbali
Afrika na katika nchi nyingine duniani. Tanzania ina majeshi ya kulinda
amani katika nchi kadhaa ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,
Darfur nchini Sudan na Lebanon.
Rais Kikwete yupo jijini New York nchini Marekani ambapo anaendelea vyema na ukaguzi wa kawaida wa afya yake. Picha na Freddy Maro
Wakikwa katika mazungumzo.
Wakiagana baada ya mazungumzo


EmoticonEmoticon