BONDIA Haji Juma wa Tanga
anatarajiwa kupanda ulingoni kuzichapa na Mohamed Mzungu wa Zanzibar katika
pambano la kuwania Ubingwa wa Tanzania (TPBO) kg 52 superfly la raundi 10
litakaofanyika Desemba 25 mwaka huu kwenye uwanja wa Tangamano jijini Tanga.
Mratibu wa Pambano hilo, Promota Ally Mwazoa alisema pambano hilo linatarajiwa kuwa la
aina yake kutokana maandalizi yaliyofanywa na uwezo walionao mabondia hao.
Mwazoa aliyataja mapambano ya
utangulizi kuwa ni bondia Rajabu Mahoja na Jumanne Mohamed wote kutoka mkoani
Tanga wataonyeshana kazi pambano la raundi 10 lenye uzito wa kg 57 feith
weight.
Licha ya kuwepo pambano hilo mabondia wengine
watakaozichapa ni Hamisi Mwakinyo wa Tanga atapambana na Said Mundi
litakalokuwa la uzito wa kg 59 super feather raundi 6 huku Saimon Zabron naye
atapigana na Athumani Boxers pambalo litakalo kuwa na uzito wa kg 61 Light
weight raundi sita.
Mratibu huyo alisema pambalo
lengine litakalo hitimisha raundi sita ni bondia J.J Ngotiko wa Tanga ambaye
atapanda ulingoni kuzichapa na Zuberi Kitandula litakalokuwa la raundi sita
super bantam.
Aliyataja mapambano ya mwisho
siku hiyo yatakuwa na raundi nne nne ambapo bondia Jacob Maganga atazichapa na
Mohamed Kidari pambano lenye uzito wa kg 65 light walter raundi nne wakati Juma
Mustapha atapambana na Selemani Hamza litakalokuwa la raundi nne lenye uzito wa
kg 55 super bantam.
Mratibu huyo alisema siku ya
mapambano hayo,mgeni rasmi anatarajiwa kuwa msanii nguli wa filamu hapa nchini
King Majuto.

EmoticonEmoticon