SASA KESI ZA MAPENZI HADI KWA MADOGO: MWANAFUNZI WA KIKE WA KIDATO CHA TATU ACHOMWA KISU TUMBONI NA MWANAFUNZI MWENZAKE WA KIKE KWA WIVU WA MAPENZI‏

December 19, 2013
Na Walter Mguluchuma .Mpanda Katavi
Mwanafunzi  wa kidato cha  tatu  katika shule ya Sekondari ya  Istiqama  iliyoko mjini Mpanda  Mkoa wa Katavi  (17) jinalake limehifadhiwa  amejeruhiwa  kwa kuchomwa  na kisu mara mbili tumboni  na mwanafunzi mwenzake wa kike  (15)   wa kidato cha tatu wa shule hiyo  kwa kisa cha kugombea mwanaume.
Kwa mujibu wa Kamanda wa  Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina Dhahiri Kidavashari  alisema tukio hilo  la mwanafunzi huyo kuchomwa kisu  tumboni mara mbili lilitokea hapo  Desemba 14 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili  na nusu jioni katika eneo la mtaa wa Kashaulili  mjini hapa 

Siku hiyo  ya tukio mwanafunzi huyo aliyejeruhiwa  alimtumia  ujumbe  wa  mfupi  wa simu  ya mkononi ya kumtukana mwanafunzi mwenzake wa kike wa  kidato cha  tatu wa shule hiyo ya  Sekondari ya Istiqama akimtaka  pia aache mahusiano  ya kimapenzi na mwanaume ambae ni mpenzi wake na  aliyejeruhiwa
Alisema  kutokana na ujumbe huo wa matusi  ulipelekea  siku hiyo   wanafunzi hao wa kike walipokutana kutokee ugomvi baina yao katika eneo hilo la Mtaa wa Kashaulili
 Kamanda Kidavashari alieleza ndipo wakati wa ogomvi huo  mwanafunzi huyo alipo chomwa  kisu mara mbili tumboni  hari ambayo ilimfanya apige mayowe ya kuomba msaada na watu waliokuwepo jirani na eneo hilo walifika na kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituo cha polisi cha Wilaya ya Mpanda 
Kidavashari  alisema   majeruhi  amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda akiendelea kupatiwa matibabu  huku hali yake  ikiwa inaendelea vizuri
 
Mtuhumiwa tayari amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda hapo kujibu mashitaka ya kumchoma kisu mwanafunzi mwenzake 

Chanzo sangafesto.blogspot.com

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »