MAANDALIZI YA MWILI WA ALIYEKUWA KATIBU WA CCM MKOA WA IRINGA YAENDELEA MORTUARY YA HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA IRINGA

December 19, 2013
 Mzee Teming'ombe akilia  kwa  uchungu  kufuatia  kifo  cha kijana wake aliyekuwa katibu  wa CCM mkoa wa  Iringa Emanuel Mteming'ombe aliyerafiki usiku wa   kuamkia  leo  katika Hospital ya Rufaa ya  mkoa wa Iringa alikolazwa kwa  zaidi ya siku mbili
 waombolezaji wakiwa  ktk hospital ya rufaa ya mkoa wa Iringa katika maandalizi  ya mwili  wa aliyekuwa katibu wa CCM mkoa wa Iringa  hivi  sasa
 Waombolezaji  wakishusha jeneza  la kuuweka mwili wa katibu wa CCM mkoa wa Iringa
Hili ndilo jeneza ambalo mwili wa aliyekuwa katibu wa CCM mkoa marehem Emanuel Mteming'ombe utawekwa

Mwili  huo  unataraji  kuombewa  katika kanisa la RC kichangani ama nyumbani kwake Gangilonga mjini Iringa kabla ya  kuondoka mida ya saa 10  jioni kwenda Rujewa Mbarali mkoa  wa Mbeya kwa mazishi yatakayofanyika  kesho  saa 5 asubuhi 

katibu  huyo alifariki dunia majira ya saa 8 hivi  usiku  wa Desemba 19 usiku  wa leo baada ya kulazwa katika Hospital ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa kwa tatizo  la figo na Athima 

Mungu ailaze  roho  yake mahali pema peponi Amina

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »