MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Tanga (CCM)Kassim Mbuguni amesema endapo vijana watajituma na kuithamini michezo itaweza kuwa mkombozi wao wa baadae pamoja na jamii zao kwa ujumla.
Mbuguni alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na vijana wa Kata ya Ngamiani Kusini katika ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM)Abdi Makange ya kukagua jumuiya hizo na kusikiliza kero za wananchi.
Alisema michezo ni ajira ya kipekee ambayo inaweza kuwainua vijana kimaisha lakini itatokana na juhudi binafsi zao kwa kuzingatia sheria
zilizowekwa pamoja na kuwaepusha kukaa vijiweni ambapo hutumia muda mwingi kufikiria vitendo viovu.
Aidha alitoa wito kwa vijana hao kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mashindano mbalimbali ya vijana ambayo huanzishwa wilayani hapa lengo
likiwa ni kuibua vipaji vyao ili baadae waweze kuonekana na timu kubwa.
“Michezo ni maisha na ajira ya kipekee ambayo inaweza kuwakwamua na umaskini mlionao hivyo nawapeni changamoto ya kuwa
kuanzia sasa mshiriki kwenye michezo na matunda yake mtayaona “Alisema Mbuguni.
Katika kuhakikisha inaipa msukumo mkubwa wa michezo kwa vijana hao aliwakabidhi vijana wa tawi la Brazili “Yeboyebo”wilayani hapa seti
moja ya jezi lengo likiwa ni kuwapa motisha kushiriki kwenye mashindano mbalimbali
EmoticonEmoticon