*WAZAZI NA WALEZI WAASWA KUWAPELEKA WATOTO WAO KUPATA VITAMIN A

December 05, 2013


Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Vincent Assey akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu mpango wa utoaji matone ya vitamin A ya nyongeza kwa watoto walio katika umri wa Miezi 6 hadi mitano, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Hassan Silayo.
***************************************************
Na Fatma Salum wa  THE GOVERNMENT OFFICIAL BLOG, 
Wazazi na Walezi wamesisitizwa kuwapeleka watoto wenye umri wa Miezi sita hadi miaka Mitano kupata matone ya vitamin A yanayotolewa kwenye vituo vya Huduma za afya Kote nchini.

Msisitizo huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Lishe toka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Vincent Assey wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.

Dkt. Assey alisema  kuwa zoezi la utoaji matone ya vitamin A kwa watoto linalofayika mara mbili kwa mwaka kila mwezi juni na disemba huenda sanjari na utoaji wa dawa za Minyoo kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja hadi miaka mitano.


Dkt. Assey alisisitiza kuwa matone hayo ni Muhimu kwa watoto kwani yanasaidia katika ukuaji,maendelezo ya afya na uhai wa mtoto.

“Ni muhimu kwa wazazi na walezi wafahamu kuwa, vyakula tunavyokula havikidhi mahitaji ya vitamin A mwilini kwa Mtoto, kwani mahitaji yao ni makubwa hivyo watoto hawana budi kupewa matone ya vitamin A mara mbili kila mwaka ili kukidi mahitaji hayo” Alisema Dkt. Assey.

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sayansi ya Chakula na Lishe kutoka Taasisi a Chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Elifatio Towo alisema kuwa watoto walio katika umri wa Miaka Mitano wanapaswa kupewa vyakula vyenye Vitami A kwa Wingi kama Mboga za Majani ,Matunda, Dagaa, mafuta ya Mawese na Maini ili kuwaongezea vitamin hiyo isiyotengenezwa na Mwili hivyo ni lazima itokane na vyakula.

Aidha Dkt. Towo aliongeza kuwa madhara yatokanayo na upungufu wa vitamin A mwilini ni pamoja na kutokuona vizuri kwenye Mwanga hafifu, upofu, maradhi ya Mara kwa Mara na Vifo vya watoto, hivyo ili kupambana na tatizo hilo yapaswa kuzigatia unyonyeshaji sahihi wa watoto,ulaji wa vyakula vyenye virutubisho na watoto kupatiwa matone ya vitamin A.



Takwimu za kitaifa juu ya demografia na afya ya jamii (Demographic and Health Survey) za mwaka 2010 zinaonesha kuwa hapa nchini upugufu wa Vitamin A unaathiri asilimia 33 ya watoto walio chini ya Umri wa miaka 5 na Asilimia 37 ya wanawake walio katika Umri wa Kuzaa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »