Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya wasanii wa muziki wa Kizazi kipya 'Bongo Flava',
walioshiriki katika kuandaa wimbo wa M Zinduka unaohamasisha kushiriki
katika kampeni mpya ya Malaria inayokwenda kwa jina la M Zinduka, baada
ya kuizindua rasmi jana usiku kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Kuzuia Malaria inayojulikana
kama ‘M-Zinduka’ inayoendeshwa kwa pamoja kati ya Kampuni ya Simu za
Mkononi ya Vodacom, Tanzania House of Talents na Malaria no more.
Wasanii hao wakiimba wimbo wao waliorekodi wa kampeni ya kuzuia malaria.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Vodacom.
Picha zote kwa hisani ya Sufianimafotoblog
EmoticonEmoticon