Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inakamilisha raundi ya kumi na moja leo kwa mechi tatu huku Yanga ikiwa mwenyeji wa Mgambo Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa
mwenyeji wa mechi kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons. Rhino Rangers na JKT
Ruvu zitacheza katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Raundi ya 12 ya ligi hiyo itaanza Oktoba 31 mwaka huu
kwa mechi kati ya Simba na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
wakati Novemba Mosi mwaka huu kutakuwa na mechi kati ya Yanga na JKT Ruvu
kwenye uwanja huo huo.
Novemba 2 mwaka huu kutakuwa na mechi nne; Mgambo
Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Tanzania Prisons na
Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar
es Salaam), na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi hiyo itakamilika Novemba 3 mwaka huu kwa mechi
moja ambapo Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo
zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union,
Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs
Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City
wakati Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

EmoticonEmoticon