MWENGE FC YAONYESHA NIA YA KUCHEZA LIGI KUU ZANZIBAR MSIMU UJAO

October 29, 2013
Na Masanja Mabula -Pemba
Timu ya soka ya Mwenge imeanza kuonyesha nia ya kutaka kurithi nafasi ya Timu ya Jamhuri kucheza ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu ujao baada ya kuifundisha soka timu ya Maendeleo Manta (Wazee wa Kununua ) mabao 2-1 katika mfululizo wa michezo la ligi daraja la kwanza Taifa Pemba uliofanyika kwenye uwanja wa Polisi Finya .
Mwenge ambayo kwa sasa inashika nafasi ya Pili kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha alama 16 ikiwa nyuma ya wanajeshi wa H/Rock wenye alama 19 iliutawala mchezo kwa dakika zote .

Katika Mpambano huo uliochezeshwa vyema na mwamuzi Asaa Ali ilishughudia mchezaji Idd Ramadhaman akiinyima bao la kuongoza timu yake ya mwenge manao dakika ya 25 baada ya kushindwa kuunganisha vyema mpira uliopigwa na Mchezaji Ali Salim  .

Wakiutumia msemo wa kwamba "Penye fungu ndipo paongezwapo " Mwenge walifanikiwa kuandika bao la kwanza katika dakika ya 42 ya kipindi cha kwanza kupitia mchezaji Idd Ramadhaman baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Maendeleo Manta .

Mwenge walifanikiwa kuongeza bao la pili katika dakika ya 53 kwa bao la kichwa lililofungwa na mchezaji Ali Salim Kareka  ambaye alifunga bao hilo baada ya kuunganisha vyema  kona iliyochongwa na Madenge kutoka winga wa kushoto .

Nalo bao la kufutia machozi la timu ya Manedeleo Manta lilipatikana katika dakika 66 likifungwa na Mchezaji Massoud Ali kwa shuti kali la Mguu wa Kushoto kufuatia uzembe uliofanywa na walinzi wa Timu ya Mwenge .

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »