Na Oscar Assenga, Tanga.
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umesema
hivi sasa hauna mpango wa kutafuta kocha mpya badala yake wataendelea na kocha
Joseph Lazaro mpaka kumalizika mzunguko wa kwanza.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Mwenyekiti wa Klabu
hiyo,Hemed Aurora “Mpiganaji”wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi
kuhusu mikakati ya kumleta kocha mpya baada ya Hemed Morroco kubwaga manyanga.
Morroco alibwaga majanga baada ya mkataba wake
kumalizika huku timu hiyo ikiwa inasuasua kufanya vizuri katika michezo yao ya
ligi kuu Tanzania bara hali ambayo wakati mwengine ilikuwa ikimuweka kwenye
wakati mgumu hasa kwa mashabiki.

EmoticonEmoticon