USAFIRI KIKWAZO KITUO CHA KUTUNZIA WAZEE CHA MWANZANGE.

October 17, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga. 
UKOSEFU wa Usafiri katika makao kwa ajili ya kuwapeleka wazee sehemu mbalimbali ikiwemo hospitalini ni miongoni mwa changamoto zinazokikabili kituo cha kutunzia wazee cha Mwanzange jijini Tanga.
 
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii katika kituo hicho,Clara Kibanga wakati akisoma taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Tanga ,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa ambaye alikwenda kituo hapo kukabidhi zawadi za sikuu ya Eid Al Hajj kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanga,Jakaya Mrisho Kikwete.

Kibanga licha ya kukabiliwa na changamoto hiyo lakini pia kuna ukosefu mkubwa wa madawa katika kituo hicho hasa pale wanapopata dharura kwa mgonjwa anayehitaji huduma ya haraka au dawa zinapokosekana katika hospitali za serikali na hivyo hulazimika kuzinunua.

Ameongeza kuwa changamoto nyingine ni uhaba wa vitanda kutokana na kuwa vilivyopo vimechakaa na ni vya muda mrefu.

Akizungumzia mafanikio ya kituo hicho,Kibanga amesema wamefanikiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa ombaomba kwa wazee licha ya kutofanikiwa kulimaliza kabisa.

Kituo hicho cha kuwahudumia wazee Mwanzange  kilianzishwa mwaka 1950 na wakoloni wa kiingereza kwa ajili ya kuwatunza wazee ambao walikuwa wafanyakazi (manamba)katika mashamba ya mkonge na chai.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »