Na Oscar Assenga,Handeni.
MKAZI wa Kijiji cha Kwedichocho wilayani Handeni mkoani Tanga Aweso Athumani (38) amemuua mkewe Saumu Athumani (24) kwa
risasi naye kujiua kwa kujipiga risasi kisongoni kwa kutumia bunduki
aina ya Gobole tukio ambalo limeacha simanzi kwa wakazi wa eneo hilo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga, Constatine Massawe alisema tukio hilo
limetokea octoba 16 mwaka huu majira ya saa kumi na moja asubuhi wakati
wakiwa nyumbani kwao ndipo alipofanya tukio hilo na kukimbilia msituni.
Massawe
alisema baada ya kukimbia msituni na ndipo alipofanya tukio hilo la
kujiua mwenyewe kwa kujipiga risasi shingoni na baadae wananchi
walipokwenda eneo hilo waliuona mwili wake na kutoa taarifa kuhusu tukio
hilo.
Kamanda
Massawe alisema baada ya polisi kufika eneo la tukio wakauchukua mwili
huo na kuufanyia uchunguzi wakagundua wamepigwa risasi na kuwakabidhi
ndugu zao kwa ajili ya taratibu za mazishi.

EmoticonEmoticon