IDARA ya Uhamiaji Mkoa wa Tanga imewataka wahamiaji haramu 32 ndani ya kipindi cha wiki mbili ambao waliingia mkoani hapa kinyume cha sheria
Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga, Sixtus Nyaki amesema tukio la kwanza lilitokea septemba 25 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili asubuhi wakati maafisa wa idara hiyo wakiwa kwenye doria walikamata wahamiaji haramu kumi raia wa Ethiopia.
Nyaki alisema raia hao walikamatiwa katika eneo la kange nje kidogo ya jiji la Tanga na kufanyiwa mahojiano ambapo ilibainika kwamba waethiopia hao waliingia nchini wakitokea nchi jirani ya Kenya na walisafiri kwa kutumia boti lililopita bahari ya hindi mpaka maeneo ya sahare jijini hapa.
Ofisa uhamiaji huyo aliwataja wahamiaji haramu hao kuwa ni Ayano Tamrat Shanko,Abraham Tafara Dobuse,Yonas Ayala Dolaso,Salamu Zalaka Wondu,Tamasgen Yohans Herano,Tasfahun Qalbiso Angore na Dababa Dante Handiso ambao wote kwa pamoja wanatuhumiwa kwa kosa la kuingia nchini kinyume na sheria ya uhamiaji.
Nyaki alisema uchunguzi bado unaendelea ili kubaini boti lililotumika na watu waliohusika kuwasaidia wahamiaji haramu kuingia nchini.
Hata hivyo alieleza taratibu za kuwafikisha mahakamani zitachukuliwa dhidi ya wahamiaji haramu waliokamatwa ambapo alisema zoezi hilo litakuwa endelevu na kutoa wito kwa wananchi na raia wema kutoa taarifa pindi wanapowaona au kuwatilia mashaka watu wa namna hiyo.
Alisema wahamiaji haramu wengine 22 walikamatwa Octoba 9 mwaka huu eneo la kisiwa cha kirui kilichopo kilomita 10 kutoka kijiji cha jasini wilayani Mkinga majira ya saa kumi na mbili jioni.
Alieleza wahamiaji haramu hao walitokea Mombasa, Kenya kwa kutumia njia ya majini wakiwa na lengo la kwenda Afrika kusini ambapo taratibu wa kuwafikisha mahakamani zinaendelea.

EmoticonEmoticon