Na Raisa Said, Bumbuli
WAZIRI wa Chakula, Kilimo na Ushirika, Injinia Christopher Chizza amependekeza kuundwa kwa menejimenti ya muda katika kiwanda cha chai cha Mponde kama njia ya kusuluhisha mgogoro uliopo katia ya wakuilima wa chai na mwekezaji wa kiwanda hicho, Kampuni ya Chai Lushoto.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mazoezi katika kata ya Mponde, Chiza
ambaye aliahidi kushughulikia mgogoro uliopo kati ya wakulima wa chai
na mwekezaji wa kiwanda cha chai cha Mponde, kilichopo Bumbuli, Tanga,
ili kiendelee kutoa huduma bora.
Alisema katika kumaliza mgogoro huo, atashauriana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu sala hilo ili kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo..
Alisema katika kumaliza mgogoro huo, atashauriana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu sala hilo ili kusaidia kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro huo..
"Nitaishauri serikali kuchukua kiwanda hicho na baadaye kuwakabidhi wananchi ambao ndio wamiliki
wa kiwanda hicho," alisema..
Mgogoro
kati ya wakulima na mwekezaji unatokana na madai ya wakulima hao
kuelezea kuwepo kwa upotevu wa fedha kiwandani na viongozi wa Chama cha
Utega kupoteza imani kwa wakulima kwa madai kuwa wako upande wa
mwekezaji ambaye walidai anaendelea kuwanyonya wakulima wa chai.
Waziri huyo pia alisema watapeleka wakaguzi kutoka serikalini kuchunguza kama kun a ubadhirifu wowote kiwandani hapo ili kuwasaidia wakulima wa chai kupata haki yao na kulisaidia zao hilo
ambalo
ndio kitega uchumi cha wakazi
wa Bumbuli lisife .
Waziri Chiza alisema kuwa ana imani uchunguzi utakaofanywa na wakaguzi kutoka serikalini utaleta majibu mazuri kwa kuwa utaonyesha kama kuna ubadhirifu na upotevu wa rasilimali zingine ndani na nje ya kiwanda hicho .
Alisema wao kama Serikali hawawezi kuendelea kuona zao la chai linaoza hivyo lazima lithaminishwe kwa kuuzwa katika viwanda vingine kwa kuwa bado mgogoro huo unaendelea na serikali inaendelea kutafuta ufumbuzi wa kumaliza mgogoro huo.
“Tutamaliza mgogoro huu kwa kupata suluhisho la haraka ili wakulima wapate haki yao ya msingi na badae waendelee kulilinda zao la chai kama ilivyokuwa zamani” alisema Waziri huyo.
Waziiri huyo alisema kuwa Chama cha UTEGA lazima kifanye mkutano mkuu ili kuadili matatizo yanayokikabili na akaahidi kuwa serikali iko tayari kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia mkutano huo.
Aidha alisema kuwa Wizara yake na Wizara ya Viwanda na Biashara wa kushiriiana na Wizara ya Mambo ya Ndani watafanya ukaguzi wa Chama hicho ili kujua kama kinaendeshwa kwa mujibu wa kanuni na sheria za Tanzania.
Wakulima hao wakizungumza katika mkutano huo wa kujadili kero mbalimbali ambazo zinawakabili, walisema kuwa wako tayari kukosa fedha kwa kipindi chote ambacho kiwanda kitakuwa kimefungwa kuliko kuendelea kunyanyaswa na wawekezaji hao.
EmoticonEmoticon