VIJANA wametakiwa kupenda michezo na kuithamini ili iweze kuwa mkombozi wao kwenye maisha yao ikiwemo kuacha kukaa vijiweni ambapo hutumia muda mwingi kufikria kutumia madawa ya kulevya.
Kauli hiyo alitolewa juzi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga(UVCCM),Abdi Makange wakati akifungua ligi ya wilaya hiyo ambayo inashirikisha timu kumi na mbili kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo.
Makange alisema michezo ni ajira ya pakee ambayo wakijipanga na kucheza kwa kujituma mafanikio yake ni makubwa sana kuliko wanavofikiria hivyo wahakikishe wanatumia vema mashindano hayo katika kukuza na kuendeleza vipaji vyao.
Aidha aliwataka vijana hao kucheza soka kwa umakini mkubwa ikiwemo kuonyesha nidhamu ya hali ya juu katika kila mchezo ili baadae waweze kupata nafasi ya kuchezea timu kubwa hapa nchini na nje ya nchini.
Awali akizungumza wakati wa ufunguzi huo,Katibu wa Chama cha soka wilaya ya Pangani(PDFA)Mussa Lyimo alisema ligi hiyo inashirikisha timu kumi na mbili kati ya hizo timu tatu zinamilikiwa na makampuni na nyengine zinajiendesha zenyewe.
Alizitaja timu hiyo kuwa ni Magic Power,Mapo Fc,Madanga Rangers,TMK Fc,Mwera City,Barcelona,Mshongo Fc,Beach Boy na Nondo Fc na kuwataka wadau wa soka wilayani humo kuvisapoti vilabu ambavyo havina wafadhili ili viweze kujiendesha.
Lyimo alisema malengo yao msimu huu ni kuhakikisha bingwa wa mkoa wa Tanga anapatikana kutoka wilayani humo kutokana na uwepo wa timu zenye uwezo wa kushindana kikamilifu ikiwemo kuleta upinzani.
MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,(UVCCM) ABDI MAKANGE AKISALIANA NA MWAMUZI WA WILAYA YA PANGANI KABLA YA KUANZA LIGI YA WILAYA HIYO HIVI KARIBUNI. |
MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE ALIYEVAA TISHETI NYEKUNDU NA MISTARI MEUPE AKIWALIMIANA NA WACHEZAJI WA TIMU ZILIZOFUNGUA PAZIA LA MASHINDANO YA LIGI YA WILAYA YA PANGANI |
MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE WA KWANZA KUSHOTO WALIOSIMAMA AKIWA NA MOJA KATI YA TIMU ZA WILAYA YA PANGANI. |
EmoticonEmoticon