WAZIRI wa Uchukuzi,Dr.Harrison Mwakyembe amesema wizara yake haitasita kuwachukulia hatua wahujumu wa miundo mbinu ya reli ikiwemo kuhakikisha wana kamatwa na kuwachukulia hatua kali zidi yao ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo.
Mwakyembe alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akizungumza katika kikao kilichokuwa kikuhusu mpango wa serikali kwenye sekta ya uchukuzi ambacho kiliwajumuisha wadau kutoka kila wilaya ,wizarani pamoja na wazawa waliopo nje ya mkoa wa Tanga.
Alisema wananchi wa Tanga waelewe kuwa miundo mbinu ya reli ni muhimu sana katika kufanikisha maendeleo yao hivyo watakikishe wanaitunza kwa sababu ni gharama kubwa kuitengeneza na kuiomba mikoa iwasaidia katika suala hilo ili iweze kuwa salama.
"Reli yetu imeonekana kuny'ofolewa kuanzia eneo la Mombo,Mkomazi kuelekea Taveta hakuna kitu sasa nasema mtu atakaye igusa reli akimkamata atamnyoa nywele kwa chupa....hakuna sababu kwani uhujumu wake unaipa hasara kubwa serikali hasa katika harakati zake za kuwaletea maendeleo wananchi "alisema Mwakyembe akisisitiza hatakuwa na msamaha kwa watu wa aina hiyo.
Akizungumzia huduma za usafiri wa ndege mkoani hapa,Dr.Mwakyembe alisema mkoa wa Tanga umeonyesha mabadiliko makubwa sana katika kipindi cha kuanzia mwaka 2007 hadi 2013 kwa watumiaji wa huduma za ndege kutoka watu 7700 mpaka 20200 wanaotumia huduma hiyo.
Alisema serikali mpango wa kuwekeza kwenye kiwanja hicho kwa kukiimarisha ikiwemo kukiongea urefu ili ndege kubwa zenye uwezo wa kubeba abiria 70 ziweze kutua mkoani hapa na kuwataka wawekezaji wenye nia kuwekeza kwenye kiwanja hicho wajitokeze.
Aidha aliwaomba wawekezaji waelewe nguvu kubwa ya usafiri wa anga kuja Tanga kwa sababu wanapoendeleza miundo mbinu ya ndege wakati huo huo kuna ukarabati na zote zinafanyika na hivyo kutatoa nafasi ya kuzikaribisha sekta nyengine binafsi.
Kwa upande wake,Mbunge wa Jimbo la Korogwe mjini,Yusuph Nassir alimuomba waziri mwakyembe kuangalia uwezekano wa uimarishaji wa kiwanja hicho uendane sambamba na uwanja wa ndege wa Tanga uwe wa kushusha mizigo ili watu wakinunua mizigo kutoka nchi za dubai na sehemu nyengine ili kutumia uwanja huo hasa wafanyabishara wa kanda ya kaskazini na mikoa ya jirani.
Akitolea ufafanuzi suala hilo,Waziri Mwakyembe alisema suala hilo ni zuri na kuiagiza mamlaka ya uwanja wa ndege hapa nchini (TAA)kulifanyia kazi hilo ikiwemo kuangalia upana wa eneo husika baadae amuwasilishie katibu mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Octoba mosi.
EmoticonEmoticon