Hifadhi ya Taifa TANAPA imewataka wananchi waishio karibu na hifadhi za wanyama pori nchini kubadilika na kuacha tabia ya kuishi kimazoea badala yake wawe wabunifu kwa kupanda mazao ambayo hayashambuliwi na wanyama waishio katika maeneo mbalimbali ya mbuga za wanyama.
Meneja Ujirani Mwema Taifa, Ahmed Mbugi alisema endapo wakazi wa maeneo jirani watapanda mazao kama ufuta,pilipili za kuwasha pamoja na miti ya kutanda ili kuzuia njia za wanyama kupita kwenye maeneo yao.
Alikuwa akizungumza katika mahojiano wakati wa mafunzo ya uandishi wa masuala ya Hifadhi ambayo yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Vijijini na Mazingira Mkoani Tanga (TARUJA) na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wilayani Pangani hivi karibuni.
Alisema kuwa hatua hiyo itasaidi kupunguza uharibifu wa mimea unaofanywa kwa sasa na wanyama hao ikiwemo kuangusha minazi pamoja na kuharibu mazao yao mengine kutokana binadamu kufanya shughuli za kilimo kwenye njia za wanyama.
“njia pekee ya kumaliza tatizo wananchi kulalamikia kuwa uharibifu wa mazao yao na wakati mwingine wanyama hao kuingia ndani ya nyumba ni kuhakikisha mnapata mazao ambayo yatasaidia wanyama kutofika kwenye maeneo ya watu”alisema Mbugi.
Naye Mwenyekiti wa kijiji cha Buyuni Kitopeni ambacho kimezungukwa na Hifadhi pande zote na Bahari uapnde mwingine, Diwani Akida alisema kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu zaidi ya minazi 770 imeangushwa na wanyama hao.
Akida alifafanua kuwa kuku 64 wamechukuliwa na tembo huku mbuzi 71 wakiliwa na simba wakiwa kwenye mabanda yao hasa nyakati za usiku na kuleta kero kubwa kwa wanakijiji waoishi maeneo ya jirani.
Alisema wao kama kijiji atua za awali walizochukuwa za kukabiliana na wanyama hao nyakati za usiku wamekuwa wakiwasha moto kwa kufunga makuti makavu ili kuwaogopesha wanyama kutoingia kwenye makazi yao kuwadhuru wao na mifugo yao.
Shabani Omary mkazi wa kijiji cha Saadani alisema kero kubwa ni nyani na ngili kuingia kwenye makazi yao na kuchukua vyakula hasa katika kipindi cha ukame .
Mwenyekiti wa kijiji cha Saadani,Mohamedi Saidi alieleza kuwa vijiji vilivyoathirika na uvamizi wa wanyama hao kuwa ni mbwebwe, uvinje pamoja na marumbi .
Ofisa wanyamapori wa wilaya Burhan Ngulungu alisema ujangili umekithiri kwa kiasi kikubwa kutokana na kutokuwepo kwa poli la akiba .
Hata hivyo alibainisha kuwa kwa sasa wamepanga mpango mkakati wa kuhakikisha wanalinda ili kupunguza madhara ya wanyama hao.
EmoticonEmoticon