MAMIA ya wakazi waTanga wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, leo wameshiriki katika mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiomoni, jijijini Tanga, George Mayalla aliyefariki juzi katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kutokana na maradhi ya kansa ya ubongo.
Akizungumza katika mazishi hayo, Gallawa aliwataka viongozi wa Vyama vya Siasa na Serikali Mkpani hapa kujenga mashirikiano ya dhati kati yao na wananchji ili kuleta maendeleo ya haraka katika maeneo yao.
Gallawa alisema kata ya Kiomoni umesifika na kupata maendeleo kunatokana na jitahada za marehemu Mayala ambaye hakuchoka kuwashirikisha wananchi katika masuala ya maendeleo shirikishi.
Alisema enzi za uhai wake, marehemu Mayalla alitumia muda wake mwingi kutekeleza dhana ya maendeleo shirikishi ambapo alizishirikisha idara za serikali , taasisi na mashirika ya umma na binafsi kusukuma gurudumu la maendeleo.
Diwani Mayalla alichaguliwa kushika nafasi ya udiwani kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010 ambapo tangu kipindi hicho amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanapata maendeleo na hilo alilitimiza kwa vitendo.
Marehemu Mayalla alizaliwa mwaka 1948 mkoani Shinyanga ambapo baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari,alichaguliwa kuingia chuo kikuu cha Dar es Salaam kuanzia mwaka 1970 hadi 1973 alipomaliza na kutunukiwa shahada ya kwanza.
Mwaka 1974 diwani Mayalla alichaguliwa kwa masomo ya juu katika chuo kikuu cha Nairobi ambako alihitimu digrii ya maendeleo na mipango miji.
Baada ya kufuzu masomo yake huko Nairobi, Kenya Mayalla aliajiriwa mkoani Dar es Salaam mwaka 1975 kama Ofisa Mipango Miji.
Mwaka 1978, Mayalla alihajishiwa Mkoani Tanga ambapo aliajiariwa kuwa Ofisa Mipango Miji wa Manispaa ya Tanga mpaka 1988 alipostaafishwa na kuwa mkulima huko Kiomoni, nje kidogo ya jiji la Tanga.
Katika mwaka 1994 hadi 2001, aliteuliwa kuwa mshauri wa kujitegemea wa Mamlaka ya Hifadhi ya Mazingira katika Manispaa ya Tanga.
Kulingana wa wasifu wa marehemu, Mayalla alipata kushika nyadhfa mbalimbali katika Halmashauri na baadaye Jiji la Tanga hadi anakutwa na mauti.
Marehemu George Mayalla ameacha mjane mmoja na watoto saba na wajukuu 11.
Mashishi yake yalihudhuriwa na mamia ya wakazi wa Tanga wakiwemo viongozi wa Chama na Serikali ambapo Meya wa Jiji la Tanga, Mstahiki Meya Omar Ghuledi alimsifia marehemu wa weledi katika utendaji kazi akisema kwamba amewahi kufanya naye kazi kwa awamu mbili.
Alisema alipata kufanya naye kazi mwaka 1984, yeye (Ghuledi) akiwa Naibu Meya wa Manispaa na marehemu akiwa Ofisa Mipango Miji.
Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga, Halima Dendego, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga, Kassimu Mbughuni, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Kassim Kisauji, Katibu wa CCM wilaya ya Tanga, Lucy Mwiru na Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa, Shekimweri na viongozi wengine mbalimbali.
Mwenyezi Mungu aiweke mahala pema peponi roho ya marehemu Mayalla. Amin
EmoticonEmoticon