TANGA WALAANI COASTAL KUFANYIWA VURUGU.

September 04, 2013
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
WAPENZI na Mashabiki wa soka mkoa Tanga wamelaani vikali kitendo cha Mashabiki na Wanachama wa Yanga kufanya vurugu katika mechi ya Ligi kuu Tanzania bara kati ya Coastal Union na Yanga iliyochezwa mwishoni mwa wiki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuzitaka mamlaka husika kutolifumbia macho suala hilo.

Mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao 1-1,ambapo wakati mwamuzi akipuliza kipenga cha mwisho kulizuka vurugu ambacho ziliwashangaza mashabiki wa soka waliofika kuuangalia mchezo huo kwa kitendo cha wachezaji wa Yanga kuwafanyia vurugu wachezaji wa Coastal Union.

Licha ya mashabiki hao kuwashambulia wachezaji lakini pia walilivamia basi la Coastal Union na kufanya uharibifu mkubwa ikiwemo kulivunja vioo jambo hilo halipaswi kuachwa lipite hivi hivi bali lazima likemewe na klabu ya Yanga iwajibike kutokana na kuwa mashabiki wao ndio waliofanya vurugu hizo

Akizungumzia suala hilo,Katibu Mkuu wa Zamani wa Coastal Union,Salim Bawazir alilaani sana kitendo hicho ambacho kilifanywa na mashabiki hao pamoja na kushangazwa na ukimya wa shirikisho la soka hapa nchini TFF kwa sababu jambo hilo haliitaji Coastal Union
kuwaandikia barua wala kulalamika bali ni kitu ambacho wanakijua hivyo tulitegemea wangechukua uamuzi wa haraka kwani mashindani hayo yana ugenini na nyumbani.

Bawazir alisema shirikisho la soka nchini TFF lisitoe nafasi kwa wapenzi wa timu hizo kushambuliana kwa sababu hatimayake yanaweza kutokea maafa makubwa sana alitolea mfano kwa timu ya Yanga ilifaniywa vurugu kubwa kabuku,Coastal Union na kabuku wapi na wapi
alisisitiza bawaziri.

Aidha alitolea mfano wa timu ya Yanga kufanyiwa vurugu mlandizi,Je watasema timu ya Simba ndio iliwashambulia?Katibu huyo alisisitiza kwa kuzitaka klabu hizo kuweka mahusiano mazuri ili kuepusha vurugu na ni vyema Yanga katika hili wakawa waungwana na kulikemea na TFF kwa sababu walikuwa uwanjani wachukue hatua kwani itawasaidia

Katibu huyo alisema watu wa Tanga mjini ni wastaarabu sana na wataendelea kuichunga heshima ya mkoa huu kwa kutokuwafanyia vurugu Yanga na timu yoyote itakayokuja kucheza kwenye uwanja wa Mkwakwani pamoja na kuwasihi sana viongozi wa Yanga wasitetee kwa njia yoyote ile vurugu hizo bali walaani hii itasaidia TFF kwani itakuwa imetoa msaada mkubwa kwenye maamuzi yake.

Wakati huo huo,Bawazir alisema anashangazwa na suala la Kocha mkuu wa timu ya Taifa(Taifa Stars) Kim Poulsen kutowajumuisha kwenye kikiso hicho wachezaji kama Shabani Kado,Hassani Banda na Hamadi Juma katika timu ya Taifa kutokana na uwezo walionao wangeweza kuisaidia timu hiyo hasa kwenye mechi zake hali hiyo inaonekana kama wachezaji wana uwezo mkubwa lakini hawachezi Simba wala Yanga hawawezi kuchaguliwa timu ya Taifa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »