TANAPA KUANZISHA VIVUTIO VYA ASILI KWENYE VIJIJI.

September 04, 2013
NA RAISA SAID,PANGANI
HIFADHI za Taifa ya Saadani (Sanapa)  inatarajia kuanzisha miradi ya vivutio vya asili vilivyoko kwenye vijiji vya maeneo yanayozunguka  hifadhi hizo ili  kuleta  maendeleo  ya  haraka  na  kuongeza  uchumi kwa  jamii inayozunguka hifadhi hizo .
Kwa mujibu  wa Muhifadhi  mkuu  wa  Hifadhi ya Saadani Hassan  Nguluma  alisema  miradi  hiyo  ni sehemu  ya  mipango  waliyokuwanayo  ya kuhakikisha  vijiji vinavyopakana  na  hifadhi  vinanufaika .
Hayo  yalisemwa  wakati wa  mafunzo  ya  uandishi  wa  masuala  ya hifadhi  yalioandaliwa  na  Chama  Cha  Waandishi  wa  Habari za  Vijijini  na  Mazingira (Taruja) na Shirika  la Hifadhi  za  Taifa  (Tanapa) yilayani  pangani  hivi  karibuni.
 “Nia yetu ni kuona wanachi wananufaika na raslimali walizonazo  kwa kuweka utaratibu wa kila maeneo kutangaza vivutio walivyonavyo zaidi ya wanyama walioko kwenye hifadhi basi wajionee mila na tamaduni zilizoko sehemu husika “.Alisema Muhifadhi  huyo.
Awali  Mwenyekiti  wa  Taruja  George Sembony alisema  kuwa lengo  la kuanzisha  chama  hicho  ni  kukuza  tasnia  ya  habari  kwa  kuongeza  ujuzi na  ufanisi  kwa  watendaji  wake  pamoja  na  kuwapa  uelewa  waandishi  juu ya  kuandika  habari  za  vijijini.
Alisema  kuwa   chama  hiki  hakikuanzishwa  ili kukinzana  na  vyama  vingine  vya  waandishi  bali  hiki  kinasaidia  katika  kuyashughulikia  masuala  moja  moja  kwa  undani  badala  ya  kuyashughulikia  kwa  ujumla .
Hata  hivyo  alisema pamoja  na  changamoto  ya  mbuga  ya  Saadani  ambayo  ndiyo  iliyowasukuma  kuomba  mafunzo  hayo  ya  siku nne yataweza  kuwapa  uelewa  zaidi  juu ya  changamoto hizo  nakuongeza  kuwa  japokuwa  mbuga  hiyo  ni mpya  napengine  wananchi  wa  eneo  hili  bado  hawajaweza  kuona  faida  ya  kuwepo  kwa  mbuga  hiyo.   
Alisema  kuwa  anaamini  kuwa  sio wote  waandishi  wanaelewa  faida  ya  kuwepo  kwa  mbuga  hiyo  kwa  maendeleo  na  ndio  maana  mambo  ambayo  yanarushwa  hewani  ni malalamiko  ya  wananchi  dhidi  ya  watendaji   wa  mbuga  hizi  ambao wanatimiza  wajibu  wao  kwa  mujibu  wa  sheria  au dhidi ya  wanyama  ambao wanaonekana  kuwa  hawana  faida  bali wanaharibu  mazao.
 Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Hussein Mselo alisema kuwa bado wananchi wa maeneo hayo hawana muako wa kutangaza vivituo vilivyoko kutoka na kukosa uwelewa wa taratibu za uendeshaji wa vivutio hivyo.
Alisema kwa sasa waandaa utaratibu wa kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananchi  wa maeneo ya jirani yenye vivutio hivyo ili kujua umuhimu wake pamoja na fursa zilizopo ili waweze kuiongezea kipato kitakacho saidia kijiji na wananchi wake.
   

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »