MSANII wa muziki wa Bongo Fleva hapa nchini,Kassim Mganga amesema wimbo wake wa "I Love You" ambao aliuachia mwezi uliopita anaamini utafanya vizuri na kuweza kumpa mafanikio makubwa kama zilivyokuwa zilizopita.
Mganga ambaye anatamba na wimbo wake wa "Ndoa Ndowano"ambao uliweza kuutikisha anga ya bongo fleva hapa nchini kutokana na aina ya mashairi aliyoyatumia kwani amepania kuutangaza mziki wake kitaifa na kimataifa zaidi.
Akizungumza na Blog hii ,Msanii huyo alisema wimbo huo unazungumzia upendo kwa ujumla hasa ukihusisha watu wawili wanaokuwa wakipendana kwa thati na kuelezea mikakati ya video yake upo mbioni kuiachia.
Aliongeza kuwa wimbo huo umetayarishwa na studio za Mazuu ambapo pia aliitaka serikali kutekeleza kwa vitendo ahadi zake za kuwasaidia wasanii wa mziki huo kwani wengi wao wanashindwa kupata haki zao za msingi kutokana na mifumo iliyopo.
Mganga alitoa ushauri kwa wasanii chipukizi kuwa makini kwa sababu mziki hivi sasa ni biashara hivyo wanapotaka kufanya mziki wajipange vilivyo na sio kukurupuka pamoja na kuwataka wasanii wakubwa kuacha kuwabagua wasanii hao bali washirikiane ili kuweza kusukuma mbele guruduma la maendeleo yao.

EmoticonEmoticon