KATIBU Mkuu wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Kassim El
Siagi (aliyekaa pichani juu)amesema mechi yao na Simba SC imewaachia pigo licha ya kuibuka na ushindi
kutokana na kuwasababishia majeraha washambuliaji wawili mahiri katika timu
hiyo baada ya kuumia kwenye mchezo huo.
Akizungumza na Blog hii,El Siagi alisema mechi hiyo ilikuwa nzuri
kutokana na wao kuibuka na ushindi lakini wakajikuta pia wachezaji wake hao
wakipata majeraha madogo madogo ambayo watalazimika kuyatibu kabla ya kuanza
msimu mpya wa ligi kuu hapa nchini.
El Siagi aliwataja washambuliaji hao kuwa ni Crispian Udulla
na Keneth Masumbuko ambao kila mmoja kwa wakati wake waliweza kutoa mchango
mkubwa sana ambapo masumbuko aliifungia Coastal Union bao la ushindi kwenye
mechi yao na URA wakati Crispian Udulla aliweza kuwa mwiba kwenye mecho ya na
Simba kwa kuifungia timu hiyo bao.
Aliongeza kuwa malengo yao makubwa ni kucheza mechi nyengine
ya kirafiki Iddi Mosi na timu nyengine ambayo wataitangaza baadae baada ya
kumalizia mazungumzo yao ambapo yakienda vizuri watacheza na Yanga.
"Malengo
yetu msimu ujao ni kuhakikisha tunacheza ligi kwa mafanikio makubwa
ikiwemo kuchukua ubingwa wa ligi hiyo kwani hilo linawezakana kutokana
na uimara wa kikosi hicho na mshikamano uliopo miongoni mwao "Alisema El
Siagi.
Katibu huyo alisema timu hiyo msimu ujao itakuwa tofauti na
vile inavyofikiriwa na wadau wa soka hapa nchini kwani usajili ambao wameufanya
na wanaotarajiwa kuufanya utakuwa kielelezo tosha cha timu hiyo kuelekea
maandalizi yao.
| UHURU SELEMAN HUYO AKICHEZA KWA STAIL WAKATI WA MAZOEZI LEO. |
| MAZOEZI SIO MCHEZO. |
| KIKOSI CHA COASTAL UNION KIKIWA MAZOEZINI JANA UWANJA WA MKWAKWANI. |
EmoticonEmoticon