STARS ILIYOFUNGWA UGANDA SIO YENYEWE BALI NI MZIZIMA UNITED.

July 31, 2013
KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA (TAIFA STARS).
Na Oscar Assenga, Tanga.
KATIBU Mkuu wa Zamani wa Coastal Union,Salim Bawazir amesema timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”iliyofungwa na Uganda katika mashindano ya Chan ni Mzizima United na sio timu ya Taifa kwani timu hiyo bado haijachaguliwa.

Bawazir ambaye pia ni mdau wa soka mwenye heshima kubwa sana katika klabu ya Coastal Union ya Tanga alisema ili tuweze kuwa na timu bora ya Taifa lazima kuwe na mashindano yatakayojumuisha mikoa yote ya Tanzania kama ilivyokuwa Taifa Cup.

Aliongeza kuwa mashindano hayo yachezwe katika kituo kimoja kwenye mkoa wa Dar es Salaam ili kuweza kumpa urahisi Kocha Mkuu wa timu ya Taifa aweze kuchagua timu bora ambayo italeta mafanikio kwenye mashindao mbalimbali ndani ya nchini na nje.

Katibu huyo aliongeza alishauri pia kuwepo kwa mashindano ya Jimbo Cup ambayo yatahusisha timu kutoka wilaya mbalimbali kwenye mikoa na kupata timu nzuri itakayopata ridhaa ya kucheza mashindano ya Taifa Cup kwa mafanikio ili kumpa urahisi kocha mkuu

kuangalia wachezaji wazuri kwa ajili ya timu za Taifa za Vijana na wakubwa.

Alisema kutokana na muundo wa sasa wakuchagua timu ya Taifa kupitia mashindano ya Ligi kuu inakuwa ni vigumu sana kupata wachezaji wenye vipaji vizuri kwani wachezaji wanaotegemewa sana ni kutoka vilabu vya Yanga na Simba aambapo kwa mtindo huo wachezaji wengi wanatoka mkoa mmoja wa Dar es Salaam wakati nchi ya Tanzania ina mikoa 26.

Kwa mtindo wa kutegemea kupata timu ya Taifa kupitia mashindano ya Ligi kuu haitoshi lazima shirikisho la soka libuni mashindano mbalimbali ambayo yatashirikisha mikoa yote ya Tanzania kama FA Cup na vile vile wayatilie mkazo mashindano ya ligi daraja la kwanza kwa kuangalia wachezaji kwani ligi hiyo imepuuzwa kwa kutokupelekwa mwalimu mkuu wa timu ya Taifa kuangalia vipaji vipya.

Akizungumzia suala la Yanga kugoma kuingia mkataba  wa kuonyeshwa michezo yao na Kampuni Television ya Azam alisena Yanga wao wajitoe  lakini timu zingine  zikubali kuwa na mkataba na kampuni hiyo.

Alisema kama Yanga wana mikataba ya ufadhili na makampuni mengine na mara nyingi sana kusalimu kwa kuwakubalia baadhi ya  maamuzi yao ndio tatizo, Kampuniya Azam na TFF wakubali ufadhili huo na waitoe Yanga michezo yao isionyweshwe katika kituo cha Televison ya Azam, timu zote zilizobaki zinahitaji ufadhili zaidi ni vyema makampuni mengi ya ndani na nje yakatoa ufadhili ili kuondoa matabaka katika ligi kuu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »