POOL Table Tanga kuanza kutimua vumbi leo.

July 04, 2013
IMEWEKWA:1:12
Na Oscar Assenga, Tanga.
 MASHINDANO ya Pool Table ngazi ya Mkoa wa Tanga yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi leo kwenye ukumbi wa Fax Night Clabu na kushirikisha vilabu kumi kutoka maeneo mbalimbali mkoani hapa.
 
Akizungumza jana, Katibu wa Chama cha Pool Table Mkoa wa Tanga,(TARPA) Shabani Kibelo alisema msimu huu wamejipanga vema kuhakikisha mapungufu yaliyojitokeza mwaka jana hayajirudii katika mashindano hayo lengo likiwa ni kupata  wachezaji wazuri ambao wataunda timu mkoa huo.
 
Kibelo alivitaja vilabu hivyo kuwa ni Hai Pub Club,BP Muheza,Michael Pub,Tanga Beathing Club na Absam Pool Club ambapo vilabu hivyo vitakuwa katika kundi A huku kundi likiwa na High Way Club,Spaider Club,Carribean Club,Kijiti Club na Etu Bomba Fax Club.
 
Katibu huyo alisema mashindano hayo msimu huu yatafunguliwa na Afisa Utamaduni wa Halmashauri ya Jiji la Tanga,Peter Semfuko ambapo pia aliwataka chama hicho taifa kuhakikisha wanawaletea mapema vifaa vya muhimu ikiwemo meza za kuchezea.
 
Aidha aliwataka wadau mbalimbali wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi ili kuweza kushuhudia mashindano hayo ambayo mwaka huu yanatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu shiriki kufanya maandalizi mapema.
 
Mwisho.

 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »