Coastal haina mpango wa kumsajili mlinda mlango mwengine-Binslum

July 01, 2013

Na Oscar Assenga,Tanga.
 
MKURUGENZI wa Ufundi wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga,Nassoro Hemed “Binslum amesema timu hiyo haina mpango wa kumsajili mlinda mlango mwengine isipokuwa waliopo wakishirikiana na Shabani Kado.
 
Kauli hiyo ya Binslum inafuatia taarifa ambazo zimekuwa zikieleza kuwa uongozi wa klabu hiyo wana mpango wa kumsajili aliyekuwa mlinda mlango wa Simba Juma Kaseja katika kipindi hiki na kusema taarifa hizo hazina ukweli wowote ule.
 
Binsulum alisema wanachokifanya hivi sasa ni kuangalia wachezaji wenye uwezo wa kuweza kuiletea mafanikio timu hiyo na sio majina kwani wapo wachezaji wa aina hiyo ambao hawaweze kuwa msaada katika timu.
 
Alisema kuelekea msimu mpya wameimarisha safu ya walinda milango ambapo Shabani Kado atasaidiana na Said Rubawa aliyesajiliwa kutoka Oljoro JKT na Mansour A.Mansour ambaye walimpandisha kutoka katika kikosi chao cha pili chini ya umri wa miaka 20.
 
Mkurugenzi huyo aliendelea kusisitiza kuwa hawajafanya mazungumzo yoyote na Juma Kaseja pia hawana mpango nae ambapo wao wanasajili kwa mipango lengo lao likiwa ni kupata mafanikio kwenye msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara.
 
Alisema kabla ya kufanya usajili huo walimu walitoa mipango yao nao kama uongozi wakaona watekeleze na kueleza kuwa katika kikosi chao mchezaji huyo hana nafasi kutokana na kuwa na walinda milango mahiri.
 
Wakati huo huo uongozi klabu hiyo umemteua Hafidhi Kido kuwa mwandishi wa klabu hiyo ambaye atakuwa na jumuku la kuhakikisha taarifa za klabu hiyo zinafika kwa wakati katika vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini nafasi ambayo aliteuliwa leo(jana).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »