WAJUMBE wa CC watakiwa kujenga ushawishi kwa wafanyabiashara-RC Gallawa

June 13, 2013
Na Oscar Assenga,Tanga.
MKUU wa mkoa wa Tanga Chiku Gallawa amewataka wajumbe wa baraza la watumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra) kujenga ushawishi kwa wafanyabiashara kutumia usafiri wa majini ili kuweza kupunguza msongamano uliopo barabarani.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akifungua mafunzo ya kamati za mikoa za baraza la watumiaji wa huduma za usafiri wa nchi kavu na majini kilichofanyika katika hotel ya Tanga Beach Resort mkoani hapa na kuhudhuriwa na wajumbe wa baraza hilo kutoka mikoa sita ambayo ni Mwanza, Arusha,Kagera,Tanga,Kigoma na Mtwara.

Gallawa alisema utumiaji huo mbali ya kupunguza msongamano barabarani lakini pia watarahisisha shughuli zao za kila siku na kuweza kufika katika maeneo husika kwa wakati uliopo kuliko kuendelea kutumia usafiri wa nchi kavu ambao huwapotezea muda.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka wajumbe wa baraza hilo kutekeleza majukumu yake sanjari na kuwa wazalendo katika kujitolea kwani kwenye maendeleo changamoto zipo hivyo wajumbe wanawajibu wa kuongeza jitihada ili kukabiliana nazo.

Awali akizungumza katika mkutano huyo,Katibu Mtendaji wa Sumatra (CC),Oscar Kikoyo alisema lengo la mkutano huo ambao uliwautanisha wajumbe kutoka mikoa sita ni kuangalia namna ya kuboresha usafiri wa nchi kavu na majini pamoja na kuishauri serikali kwenye baadhi ya mambo ili kuweza kupata maendeleo.

Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »