Na Mwandishi wetu, Makete.
Benki ya NMB imekabidhi vifaa tiba ikiwemo vitanda na mashuka katika Zahanati ya Kijiji cha Ivilikinge wilyani Makete mkoani Njombe vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo mwishoni mwa wiki, Kaimu Meneja Benki ya NMB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Willy Mponzi alisema benki hiyo kila mwaka imekuwa na utamaduni wa kutenga asilimia moja ya pato lake baada ya makato ya kodi kwa lengo la kurudisha kwa jamii.
“Msaada huu ambao leo tumekabidhi Makete pia tumekuwa tunakabidhi katika sehemu mbalimbali katika nchi yetu na huu msaada umehusisha vifaa tiba,” amesema Mponzi.
Alisema awali wakati zahanati hiyo inaanza ujenzi, benki hiyo pia ilichangia bati zenye thamani ya milioni nane.
Aidha alisema kuwa, kwa miaka kadhaa sasa NMB imekuwa ikisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi kwa kujikita zaidi kwenye miradi ya elimu ambayo inahusisha madawati, vifaa vya kuezekea lakini kwenye vituo vya afya wametoa vitanda, magodolo na vifaa vyengine vya matibabu.
"Na pia benki ya NMB tumekuwa tukisaidia nchi yetu kwa majanga mbalimbali, tunatambua kuwa ni kupitia jamii ndipo wateja wetu wengi wanapotoka," amesema Mponzi.
Naye Katibu wa Chama cha Maendeleo Makete (MDA), Award Mpandila aliishukuru NMB kwa msaada huo na kuwaomba kuendelea kuboresha mahusiano yaliyopo kati ya NMB na wananchi.
Kwa Upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana aliishukuru benki ya NMB kwa kuunga mkono jitihada za serikali na wananchi na kuwataka kuendelea kushirikiana ili kuleta tija kwa taifa.
Awali Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Kijiji cha Ivilikinge, Hassan Yusuph alisema mara baada ya wananchi kuibua mradi wa ujenzi zahanati benki ya NMB iliwasaidia bati yenye thamani ya shilingi milioni nane.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Makete, Juma Sweda aliiomba benki ya NMB kuwaunga mkono pia kwenye ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa zahanati hiyo.
Share this
Related Posts
BENKI YA CRDB KUIWEZESHA ZANZIBAR KUJENGA SHULE 23 ZA GHOROFA Zanzibar. Tarehe 21 Mei 2025: Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amei
MWENGE WA UHURU KUZINDUA KUWEKA MAWE YA MSINGI MIRADI 11 YA MAJI MKOANI TANGA YENYE THAMANI YA BILIONI 16.7 Na Oscar Assenga, TANGA JUMLA ya Miradi 11 katika Sekta ya Maji yenye thamani ya Sh.Bilioni 16,713,383,870 inata
TASAC YATOA ELIMU YA UTUNZAJI MAZINGIRA DODOMAShirika la Uwakala wa Meli Tanzania TASAC, leo tarehe 02 Juni, 2025 limetoa elimu ya utunzaji wa mazingira majini kwa w
DC SAME APIGA MARUFUKU MAJI MACHAFU YA KIWANDA KUINGIA MTONI Na Ashrack Miraji Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, amepiga marufuku mara moja utiririshaji wa maji ma
EmoticonEmoticon