OFISA MKUU WA FEDHA - AngloGold Ashanti ATEMBELEA GGML

January 29, 2024

 Na Mwandishi Wetu


OFISA Mkuu wa masuala ya fedha (CFO) kutoka Kampuni ya AngloGold Ashanti inayomiliki Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Gillian Doran wiki iliyopita alikaribishwa na kuutembelea mgodi huo uliopo mkoani Geita.

Mbali na Doran pia Meneja Mwandamizi wa Ushuru – Afrika, Jacques Labuschagne na Makamu wa Rais wa masuala ya Fedha – Afrika, Himesh Persotam pia waliitembelea GGML.

Akizungumza baada ya ziara hiyo Doran amesema ziara yao haikuwa ya kihistoria tu, kwani ilikuwa ni ziara ya kwanza ya CFO, lakini pia ilitoa maelekezo muhimu kuhusu shughuli za mgodi huo wa dhahabu wa Geita.

"Ziara hii haikuwa ya kihistoria tu, kwani ilikuwa ni ziara ya kwanza ya CFO, lakini pia ilitoa maelekezo muhimu kuhusu shughuli za mgodi huo wa dhahabu wa Geita."

Yusuph Mhando, Meneja Mazingira (aliyeupa mgongo kamera), akimfafanulia CFO wa AngloGold Ashanti Gillian Doran (wa pili kutoka kulia) namna kanuni za mazingira zinazotambuliwa na kufuatwa na GGML katika shughuli zake.
Zulu Nkanyiso ambaye ni Meneja Mwandamizi wa Mtambo wa uchenjuaji akijibu maswali kutoka kwa Gillian Doran, Ofisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti, kuhusu muongozo wa GGML wa usimamizi na uhifadhi wa takasumu (TSF).

Mhandisi wa GGML anayedhibiti ubora na viwango vya miradi, Maftah Seif akitoa maelezo zaidi kuhusu teknolojia ya hali ya juu itakayotekelezwa katika kituo kipya cha GGML chenye uhusiano na TANESCO. Mradi huo ni ushahidi wa juhudi za GGML zinazoendelea za kuboresha kuongeza ufanisi wa kiutendaji.
Gilbert Chamlonde, Meneja – uchimbaji wa kina kifupi juu ya ardhi akitoa muhtasari wa historia ya uzalishaji wa mgodi wa Nyamulilima kwa Afisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti, Gillian Doran.

Gillian Doran ambaye ni Ofisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti (katikati), pamoja na Himesh Persotam (mwisho kushoto), Makamu wa Rais: Masuala ya Fedha - Afrika, na Jacques Labuschagne, Meneja Mwandamizi wa masuala ya Ushuru Afrika, (wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja kando ya mgodi wa Nyamulilima na baadhi ya menejiment ya GGML.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »