ASILIMIA 43 YA GESIJOTO INAHITAJI KUPUNGUZWA IFIKAPO MWAKA 2030

January 24, 2024

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema asilimia 43 ya gesijoto inahitaji kupunguzwa ifikapo mwaka 2030 ili kuwezesha joto la dunia kutoongezeka zaidi ya nyuzi joto 1.5.


Amesema hatua hiyo itafanyika kwa kuongeza matumizi ya nishati jadidifu, kuongeza jitihada za kuachana na matumizi ya nishati chafuzi na kuondoa ruzuku kwa matumizi ya makaa ya mawe; kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na ushirikishwaji wa sekta binafsi na asasi za kiraia.

Dkt. Jafo amesema hayo wakati akiwasilisha taarifa ya maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Januari 2024.

Aidha, amesema kuwa mikakati ya kupunguza gesijoto, viongozi wa nchi wanachama walijadili jinsi ya kuimarisha jitihada za kupunguza uzalishaji wake hadi kubakia chini ya nyuzi joto 2.

Waziri Jafo amesema pia, majadiliano hayo yalihusu uanzishwaji wa programu ya upunguzaji wa gesijoto na haja ya kuondoa ufadhili na matumizi ya vyanzo vya nishati ya mafuta na makaa ya mawe kutokana na sababu za kuchangia katika uzalishaji wa gesijoto na uchafuzi wa mazingira duniani ambayo hata hivyo, makubaliano hayakufikiwa.

Halikadhalika, nchi wanachama kwa pamoja zimeombwa kutoa fedha kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa mpango kazi wa Kamati ya Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na kutoa miongozo na mafunzo ili kubaini mahitaji ya nchi zinazoendelea katika kuandaa na kutekeleza mipango ya taifa ya kuhimili changamoto hizo.

Ameongeza kuwa Mkutano wa COP28 umetambua uwepo wa pengo kubwa katika utoaji wa fedha na Dola za Marekani trilioni 5.8 hadi 5.9 zinahitajika kwa mwaka ili kufikia malengo ya upunguzaji wa uzalishaji wa gesi joto ifikapo mwaka 2030.

“Majadiliano katika agenda hii yalijikita katika kuwezesha upatikanaji wa teknolojia zinazohitajika kwa wakati na kwa gharama nafuu kama ilivyobainishwa katika Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi na Makubaliano ya Paris,” amesema huku akiongeza kuwa taasisi za fedha zimeombwa kuendelea kutafuta fedha kwa ajili ya uendelezaji na uhaulishaji wa teknolojia za kuhimili na kupunguza uzalishaji wa gesijoto katika nchi zinazoendelea.

Amesema kuwa ushiriki wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 28 umeiwezesha nchi kuendelea kuimarisha ushirikiano na jumuiya za kimataifa na kikanda pamoja na kuibua fursa zaidi za miradi, uwekezaji na utafiti katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira kupitia kwa Mwenyekiti wake Mhe. Jackson Kiswaga imeipongeza Serikali kwa maandalizi na kushiriki kwa mkutano huo ambao umeonesha tija.

Amesisitiza kuongeza nguvu katika kuandika maandiko ya kuomba fedha kutoka kwa nchi zilizoendelea ili zizinufaishe nchi zinazoendelea ambazo zimekuwa waathirika wakubwa wa athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kikao hicho pia kimepokea taarifa ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwasilisha taarifa kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akifafafanua jambo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga akiongoza kikao cha kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Immaculate Semesi akifafanua jambo wakati wa kkikao cha kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo, jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Kemilembe Mutasa akifafanua jambo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo, jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Ladislaus Chang'a akifafanua jambo ya utendaji wa Mamlaka kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Selemani Jafo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga wakifuatilia kikao cha kuwasilisha taarifa ya maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira jijini Dodoma leo Januari 23, 2024.
Wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Makamu wa Rais wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu maazimio yaliyofikiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) na ya utendaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuhusu mwenendo wa mabadiliko ya tabianchi, athari za mazingira na tathmini ya mabadiliko hayo kwa kipindi cha miaka 10 ijayo, jijini Dodoma leo Januari 2024.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »